Nenda kwa yaliyomo

Kashmir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Moja ya Sehemu ya mji ndani ya jimbo la wa Kashmir
Kashmir: Utemi wa kihistoria ya Jammu na Kashmir (mstari mwekundu) na mgawanyo kwa maeneo ya Uhindi, Pakistan na Uchina.

Kashmir (Kihindi: कश्मीर, Kiurdu: کشمیر) ni eneo katika kazkazini ya Bara Hindi kwenye milima ya Himalaya. Eneo hili limegawiwa kati ya Pakistan na Uhindi tangu 1947. Sehemu ndogo katika milima ya juu ya Kazkazini imevamiwa na Uchina tangu 1962.

Fitina ya Kashmir imesababisha tayari vita tatu za 1947, 1965 na 1999 kati ya India na Pakistan. Imekuwa pia chanzo cha ugaidi ndani ya Uhindi.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Kijiografia kiini cha "Kashmir" ni Bonde la Kashmir ambalo ni bonde kubwa la mto Jheam lenye rutba kati ya Himalaya ya Juu na milima ya Pir Panjal. Katika karne ya 19 bonde liliunganishwa na maeno jirani ya Jammu na Ladakh jumla 222,236 km² penye milima na chanzo cha mto Indus (Hindi). Eneo hili liligawiwa 1947.

  • Sehemu ya Kihindi ni jimbo la kujitawala ndani ya shirikisho la Uhindi linatumia jina la kihistoria "Jammu na Kashmir". Eneo lake ni km² 101,387 kuna wakazi milioni 10.1.
  • Sehemu ya Pakistan inaitwa Asad Kaschmir ("Kashmir Huru"). Eneo lake ni km² 83.888 kuna wakazi milioni 1.3.
  • Sehemu ya kichina ni Aksai Chin. Eneo hili ni jangwa baridi la chumvi lenye km² 38,000 kwenye kimo cha m 5000. Wakazi ni wachache sana.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Hadi 1947 sehemu zote za Kashmir zilikuwa eneo la dola la maharaja wa "Jammu na Kashmir". Alitawala chini ya ulinzi wa Uingereza.

Mwaka 1947 Uhindi wa Kiingereza iligawanywa kuwa madola mawili mapya ya Pakistan na Uhindi. Sheria ya Uingereza ilisema ya kwamba maeneo penye Waislamu wengi wangekuwa upande wa Pakistan na maeneo penye Wahindu wengi upande wa Uhindi. Madola ya kitemi chini ya ulinzi wa Uingereza yalitakiwa kujiunga na upande mmoja.

Maharaja Hari Singh wa Jammu na Kashmir alijaribu kutetea uhuru wa utemi wake bila kujiunga na upande wowote. Lakini Pakistan ilichochea upinzani ikadai ya kwamba eneo hili lenye Waislamu kiasi cha 70% ya wakazi ilipaswa kuwa sehemu ya Pakistan. Aliposhambuliwa na wanamgambo Waislamu waliosaidiwa na kungozwa na jeshi la Pakistan maharaja alitangaza kujiunga na shirikisho la Uhindi akaomba msaada wa kijeshi. Vita ilipiganiwa kati ya Oktoba 1947 hadi mwisho wa mwaka 1948. Tokeo lake lilikuwa mgawanyiko wa Kashmir kwenye mstari wa mapigano.

Makala hii kuhusu maeneo ya Uhindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kashmir kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.