Kanuni ya Peter
Kanuni ya Peter (kwa Kiing. Peter Principle) ni dhana iliyoanzishwa na Laurence J. Peter, ambayo inasema kwamba katika mfumo wa kiutawala, mfanyakazi hupandishwa ngazi za juu zaidi kutokana na mafanikio kwenye ngazi zilizotangulia, hadi kufikia ngazi inayomshinda ambako anaonekana hawezi kutekeleza wajibu wake tena.[1]
Dhana hiyo ilielezwa na Laurence Peter na Raymond Hull katika kitabu cha mwaka 1969 The Peter Principle. [2] Peter na Hull walikusudia kitabu hicho kiwe kejeli, [3] lakini kikawa maarufu kwani kilionekana kutoa hoja nzito kuhusu mapungufu ya mfumo wa kuwapandisha watumishi ngazi.
Kanuni ya Peter tangu wakati huo imekuwa mada ya ufafanuzi na utafiti mwingi.
Kanuni ya Peter inasema kwamba mtu ambaye ana uwezo katika kazi yake atapandishwa cheo hadi kufika nafasi ambayo inahitaji uwezo tofauti na ile alipotangulia kama mtumishi.
Mtu aliyepandishwa cheo anakosa ujuzi unaohitajika kwa jukumu jipya, atakuwa hana uwezo katika ngazi mpya, na hatapandishwa cheo tena. [4] Ikiwa mtu huyo ana uwezo katika jukumu jipya, atapandishwa tena na ataendelea kupandishwa hadi kufikia kiwango ambacho hana uwezo. Kwa kuwa hana uwezo, mtu huyo hatahitimu kupandishwa cheo tena, na kwa hubaki kukwama katika nafasi hiyo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hayes, Adam (Ago 21, 2020). "Peter Principle: What You Need to Know". Investopedia (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Peter, Laurence J., and Raymond Hull. [1969] 1970. The Peter Principle. Pan Books.
- ↑ Barron, James. "Laurence J. Peter Is Dead at 70; His 'Principle' Satirized Business", The New York Times, 1990-01-15. (en-US)
- ↑ Hayes, Adam (Ago 21, 2020). "Peter Principle: What You Need to Know". Investopedia (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-17.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)