Historia ya Tajikistan
Historia ya Tajikistan inahusu historia ya eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Tajikistan.
Eneo hilo lilitawaliwa na madola mbalimbali, hasa na Uajemi.
Uislamu ulifika huko mnamo mwaka 800 BK.
Mwaka 1868 Tajikistan ilivamiwa na Urusi na kuwa sehemu ya Dola la Urusi, halafu sehemu ya Umoja wa Kisovyet baada ya mapinduzi ya 1917. Iliitwa Jamhuri ya Kisovyeti ya Kisoshalisti ya Tajikistan.
Baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisoviet, Tajikistan ilipata uhuru wake mwaka 1991.
Kati ya mwaka 1992 hadi 1997 kulikuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilisababisha Warusi wengi kuondoka na vilikwisha kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
Baada ya mashambulio ya kigaidi ya tarehe 11 Septemba 2001 jeshi la Marekani lilipata nafasi ya kutumia vituo vya kijeshi kwa ajili ya vita katika Afghanistan.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Tajikistan kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |