Guam
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Where America's Day Begins" | |||||
Wimbo wa taifa: Fanohge Chamoru | |||||
Mji mkuu | Hagatna (Agana) | ||||
Kijiji | Dededo | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza, Kichamoru | ||||
Serikali | Eneo la ng'ambo la Marekani Donald Trump Felix Perez Camacho | ||||
Eneo la ng'ambo la Marekani Koloni la Hispania Koloni la Marekani Eneo la ng'ambo la Marekani |
1668 1898 1949 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
543.52 km² (ya 192) ‘‘(kidogo sana)’’ | ||||
Idadi ya watu - Julai 2006 kadirio - Msongamano wa watu |
170,000 (ya 186) 307/km² (ya 37) | ||||
Fedha | US Dollar (USD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
Chamorro Standard Time (UTC+10) -- (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .gu | ||||
Kodi ya simu | +1-671
- |
Guam (kwa Kichamoru: Guåhan) ni eneo la ng'ambo la Marekani (U.S. Territory of Guam) upande wa kusini wa funguvisiwa ya Mariana katika Bahari ya Pasifiki. Huhesabiwa kati ya visiwa vya Mikronesia.
Eneo la kisiwa hicho ni kilometa mraba 543.
Uchumi wa Guam unategemea kituo cha kijeshi cha Marekani pamoja na utalii.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Wakazi wa kwanza wanaojulikana ni Wachamoru walihamia miaka 4,000 hivi iliyopita.
Tangu mwaka 1668 visiwa vya Mariana vilikuwa koloni la Hispania.
Baada ya vita ya Marekani dhidi Hispania Guam ikatwaliwa na Marekani. Visiwa vya upande wa Kaskazini vikauzwa kwa Ujerumani na kuwa Mariana ya Kaskazini.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kisiwa kikatwaliwa na Japani, lakini tarehe 21 Julai 1944 Waamerika walirudi na kuwafukuza Wajapani.
Mwaka 1949 kisiwa kilipewa hadhi ya Eneo la ng'ambo la Marekani, wakazi wake wakapewa uraia wa shirikisho hilo.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Kwa sasa 37.1% ya wakazi wote (159,358) ni Wachamoru, wakifuatwa na Wafilipino (26.3%). Wachamoru wengi zaidi wanaishi Marekani bara.
Upande wa dini, 85% ni Wakristo wa Kanisa Katoliki.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]
Nchi_na maeneo ya Australia na Pasifiki |
Australia | Fiji | Guam | Hawaii | Kaledonia Mpya | Kiribati | Kisiwa cha Pasaka | Mikronesia | Nauru | Nyuzilandi | Niue | Pitcairn | Polinesia ya Kifaransa | Palau | Papua Guinea Mpya | Samoa | Samoa ya Marekani | Visiwa vya Cook | Visiwa vya Mariana ya Kaskazini | Visiwa vya Marshall | Visiwa vya Solomon | Tonga | Tuvalu | Vanuatu | Wallis na Futuna |
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guam kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |