Godoro
Godoro ni kifaa kikubwa cha kusaidia mwili kupumzika. Hutumiwa kama kitanda au kama sehemu ya kitanda. Godoro huwekwa kwenye chaga ya kitanda na kulaliwa.
Godoro huwa na kitambaa cha juu ambacho ndani yake huenda kukawa na sponji, nyasi, nywele au pamba. Godoro za kisasa huenda zikawa na maji au hata hewa iliyowekwa kwenye kifuko kisicho na vishimo na kitakachoweza kubeba yaliyomo ndani yake.
Historia ya godoro
[hariri | hariri chanzo]Godoro lilivumbuliwa na Waarabu na jina la Kiingereza Mattress lamaanisha 'kuweka chini' katika lugha ya Kiarabu.
Wakati wa vita vya msalaba, magodoro yalitumika kulalia chini. Tabia hii ilikuwa kuiga Waarabu waliokuwa wakilalia magodoro na hata mikeka iliyowekwa chini.
Magodoro haya ya hapo zamani yalijazwa nyasi, manyoya ya ndege au hata nywele za farasi.
Magodoro ya zamina kabisa yaliyoko kwa historia yaonekana kuwa na takribani miaka 77,000.
Magodoro ya kisasa
[hariri | hariri chanzo]Godoro za kisasa hujazwa kwa sponji au hata mpira (rubber) na hujulikana kama innerspring kwani huweza kupinda na kukunjika kwa urahisi. Haswa yale ya vitanda vya hospitali huwa ni innerspring, kwani vitanda vya hospitali hukunjwa ili mgonjwa apate kustareheka.
Magodoro ya kisasa huenda pia yakawa na uwezo wa kupashwa kawi ya umeme ili kuweka joto katika kitanda.
Magodoro yanaweza kuwekwa kwa vikundi tofauti kulingana na vipimo. Haya ni kama
- Godoro pacha (twin mattress): ndilo godoro ndogo kabisa kati ya magodoro yote. Kwa kawaida hununuliwa kwa minajili ya mtoto mchanga ambaye ametolewa katika kijitanda alichokuwa akilalia badda ya kuzaliwa.Huwa na kipimo cha inchi 38 kwa upana na 75 kwa urefu.
- Godoro wastani (full): hili ni kubwa kuliko godoro pacha. Hutumiwa na wanaolala pekee yao haswa wasio kwenye ndoa. Huwa na upana wa inchi 53 na urefu wa 75
- Godoro malkia: unapoingia kwenye ndoa, huenda ukaona kwamba godoro wastani halitoshi na kwa hivyo inabidi utafute godoro kubwa. Hapa ndipo walio kwenye ndoa hutafuta godoro hili ambalo litawatosha wote. Upana wake ni inchi 60 na urefu wa inchi 80.
- Godoro mfalme: ndilo kubwa kabisa na huwa na nafasi kubwa ya kulalia. Watu hulinunua kwa sababu ya starehe na huonyesha pia kuwa mtu ana kipato kikubwa. Huwa na upana wa inchi 76 na urefu wa inchi 80
Vile vile magodoro hutumika kwa starehe na kuna yale haswa ya wagonjwa ya kuzuia wapate maumivu mengi wanapolala.
- Godoro maji: hilo huwa limejazwa na maji hivi kwamba ukililalia utapata ukidundadunda kwa kurushwarushwa na maji. Watu hulinunua hili godoro kwa minajili ya starehe.
- Godoro hewa: hilo hutumiwa sana na wagonjwa walio na shida za maumivu ya mgongo. Huweza kumfanya mwenye maumivu awache kupatwa na makali mengi.
- Godoro kambi: watu wanapokita kambi hupenda kununua kigodoro kitakachotoshea kwenye hema au kambi wanapokaa.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- History of mattress Ilihifadhiwa 23 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- World's oldest mattress
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Godoro kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |