Nenda kwa yaliyomo

Fu-Gee-La

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Fu-Gee-La”
“Fu-Gee-La” cover
Single ya Fugees
kutoka katika albamu ya The Score
Imetolewa 9 Januari 1996
Muundo 12" single
Imerekodiwa 1995
Aina Hip hop, Rap
Urefu 4:20
Studio Ruffhouse Records
Mtunzi Nelust Wyclef Jean
Samuel Prakazrel Michel
Lauryn Noel Hill
Allen McGrier
Teena Marie
Salaam Remi
Mtayarishaji Salaam Remi
Certification Gold (RIAA)
Mwenendo wa single za Fugees
"Vocab"
(1994)
"Fu-Gee-La"
(1996)
"Ready or Not"
(1996)

"Fu-Gee-La" ni single ya kwanza kutoka katika albamu ya pili ya kundi zima la The Fugees', The Score. Wimbo, ambao ulitayarishwa na Salaam Remi, imemjulisha samupuli ya wimbo wa "If Loving You Is Wrong, I Don't Want To Be Right" wa Ramsey Lewis, na kiitikio chake kinatokana na "Ooh La La La" wa Teena Marie. Maremixi kadhaa ya wimbo yalifanyika ("Refugee Camp Remix" na "Sly & Robbie Remix", ambayo pia imemshirikisha Akon wakati yu bwana mdogo) pia ameonekana kwenye The Score. Hii ni single pekee ya The Fugees kupata mauzo ya hali ya juu, na ilitunukiwa dhahabu na RIAA.[1]

Muziki wa video

[hariri | hariri chanzo]

Muziki wa video wa Fu-Gee-La ulipigwa nchini Jamaika. Muziki wa video unaelezea kisa kinachohusiana na masuala ya wizi wa mapesa, ambamo kila mmoja kwenye kundi hili kachukua nafasi yake husika. Mwanzoni anaonekana Pras akishuka kwenye pikipiki na mali ya magendo. Wakati huohuo anaoneshwa Hill akivizia askari apite ili aweze kupora mzigo uliokuwa karibu naye. Mbeleni, anaonekana Jean akiwa mbioni na mwishowe wote wanakutana mahala pamoja na kuanza mbio za magari baina ya polisi na kina Fugees. Mbio zile ziliishia kivukoni ambapo kina Hill wamechelewa kufika pale kwa sababu wale mapolisi walipita njia ya mkato na kutangulia kufika kabla ya wao. Kilichofuata ni kumwaga mapesa wale mapolisi wasishughulike na wao halafu wanaonekana wakirukia boti lililokuwa likiondoka kivukoni taratibu.

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Fu-Gee-La" (Album Version) (4:15)
  2. "Fu-Gee-La" (North Side Mix) (4:15)
  3. "Fu-Gee-La" (Refugee Camp Remix) (4:24)
  4. "Fu-Gee-La" (Sly & Robbie Mix) (5:33)
  5. "Fu-Gee-La" (Wyclef's Global Acoustic Mix) (4:18)
  6. "Fu-Gee-La" (Fugi Acapella) (4:08)
  1. "Fu-Gee-La" (Album Version) (4:15)
  2. "Fu-Gee-La" (Refugee Camp Remix Instrumental) (4:22)
  3. "How Many Mics" (4:22)
  4. "How Many Mics" (Acapella) (4:16)
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-08. Iliwekwa mnamo 2010-06-09.