Nenda kwa yaliyomo

Emirates

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Emirates ni ndege kuu katika bara la Arabu, iliyo chini ya kampuni ya The Emirates Group. Ni ndege ya kitaifa iliyo mjini Dubai, miliki za kiarabuUnited Arab Emirates na inahudumu takriban wasafiri 2200 kila wiki[1] kutoka kwa kituo chake cha Uwanja wa ndege wa kimataifa ya Dubai, Terminal 3 hadi nchi 55 na kwenye bara sita.[2] Emirates iko chini ya The Emirates Group, ambayo ina waajiriwa zaidi ya 40,000, na inayomilikiwa na serikali ya Dubai.

Ndege hii iko kwenye ndege kumi bora kulingana na mauzo, wasafiri na kilomita.[3]

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Boeing 777-300ER

Ndege ya kwanza ya Emirates ilisafiri kutoka mji wa Dubai hadi Karachi mnamo 25 Oktoba 1985.[4]

Emirates ilianza kupata faida kuanzia baada ya miezi tisa. Mwaka wake wa kwanza, ilibeba wasafiri 260,000 na mizigi ya tani 10,000. Mnamo 1986, ndege hii iliongeza miji ya kusafiria kama Colombo, Dhaka, Amman, na Cairo miongoni mwa miji inayosafiria. Emirates ilianzisha ndege za kusafiri hadi London Gatwick kila siku mnamo 6 Julai 1987 kwa kutumia ndege mbili za Airbus A310. Pia, ilianzisha ndege za kuelekea mjini Singapore. Mnamo 1987, Ilianza kwenda Frankfurt kwa kupitia miji ya Istanbul, na Male.

Maendeleo

[hariri | hariri chanzo]
Emirates ilikuwa na ndege tisa za aina ya A310 mnamo 1998

Mauzo ya Emirates ziliongezeka kwa takriban milioni $100 kila mwaka, na kufikia milioni $500 mnamo 1993. Mwaka huu, ilibeba mizigo ya tani 68,000 na wasafiri milioni 1.6

Emirates ilipata mauzo ya milioni $643.4 katika mwaka wa 1994. Ilikuwa na wafanyikazi 4,000.

Terminal 3

[hariri | hariri chanzo]

Terminal 3 kwenye Uwanja wa ndege ya Dubai ilijengewa kwa matumizi ya Emirates pekee. Iligharimu bilioni $4.5 na ilifunguliwa rasmi mnamo 14 Oktoba 2008. Terminal hii inaweza kutosheleza masafiri milioni 27.

Waajiriwa

[hariri | hariri chanzo]

Emirates imeajiri jumla ya watu 28,037 hadi mwaka wa 31 Machi 2009.[5]

Mauzo na faida

[hariri | hariri chanzo]
Emirates Financial and Operational Performance[6]
Year Ended Passengers Flown Cargo carried (thousand) Turnover (AEDm) Expenditure (AEDm) Net Profit/Loss (AEDm)
31 Machi 1997 3,114.3 159.4 1,198.7 1,097.1 101.623
31 Machi 1998 3,683.4 200.1 4,089.1 3,826.7 262.413
31 Machi 1999 4,252.7 214.2 4,442.9 4,130.2 312.959
31 Machi 2000 4,775.4 269.9 5,113.8 4,812.9 300.900
31 Machi 2001 5,718.8 335.2 6,417.3 5,970.7 421.825
31 Machi 2002 6,765.1 400.6 7,274.6 6,783.7 468.231
31 Machi 2003 8,502.8 525.2 9,709.7 8,749.6 906.747
31 Machi 2004 10,441.3 659.8 13,286.3 11,602.1 1,573.511
31 Machi 2005 12,528.7 838.4 18,130.9 15,628.3 2,407.385
31 Machi 2006 14,497.5 1 ,018.5 23,050.9 20,489.6 2,474.97
31 Machi 2007 17,544.1 1,155.9 29,839.6 26,675.9 3,096.4
31 Machi 2008 21,229.2 1,282.1 40,196.6 35,121.7 5,020.4
31 Machi 2009 22,730.9 1,408.3 44,188.9 43,143.4 981.7

Kuanzia 2004, nembo ya Emirates ni Fly Emirates. Keep Discovering. Zingine zilizowahi kutumika ni kama:

  • The Finest in the Sky
  • Be Good to yourself. Fly Emirates
  • When was the last time you did something for the first time
  • Fly Emirates. Meet Dubai.
  • Fly Emirates. To over Six Continents.[7]

Miji inayosafiria

[hariri | hariri chanzo]

Emirates inahudumu ndege 1,883 kila wiki, katika miji 103 kwenye nchi 65 kwenye bara 6 kutoka kwa kituo chake mjini Dubai.

Mapumziko

[hariri | hariri chanzo]

Ndege hii ina vyumba vya mapumziko kwenye uwanja wa ndege katika miji ifuatayo:

  1. "Emirates to Launch Second Phase Operations at Dubai Airport Terminal-3 - Business News". redOrbit. Iliwekwa mnamo 2009-07-15.
  2. Emirates Announces 2009 Expansion Plan
  3. "Gulfnews: Emirates is now seventh biggest airline". Archive.gulfnews.com. 2007-11-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-22. Iliwekwa mnamo 2009-07-15.
  4. "Emirates - Company Profile on LinkedIn". Linkedin.com. 2009-07-02. Iliwekwa mnamo 2009-07-15.
  5. "Mohammed Bin Rashid inspects Emirates Group's headquarters". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-01-18. Iliwekwa mnamo 2010-01-21.
  6. "Annual Reports | The Emirates Group". Ekgroup.com. 2009-07-09. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-16. Iliwekwa mnamo 2009-07-15.
  7. "About Emirates | Emirates Advertising". Emirates. 2008-06-03. Iliwekwa mnamo 2009-07-15.
  8. http://www.emirates.com/us/english/about/news/news_detail.aspx?article=523917&offset=0
  9. http://www.emirates.com/us/english/about/news/news_detail.aspx?article=530937&offset=0
  10. http://www.emirates.com/us/english/about/news/news_detail.aspx?article=526496&offset=0
  11. http://www.emirates.com/us/english/about/news/news_detail.aspx?article=534704&offset=0
  12. Emirates has two lounges at Brisbane Airport, separate for First and Business Class passengers (only first class Emirates lounge outside of Dubai).
  13. Emirates has three lounges at Dubai Airport, separate for First and Business Class passengers and one in Terminal 1 for transit passengers.