Danubi (mto)
Mto wa Danubi | |
---|---|
| |
Chanzo | Milima ya Msitu Mweusi, Ujerumani |
Mdomo | Bahari Nyeusi |
Nchi za beseni ya mto | Romania (28.9%), Hungaria (11.7%), Austria (10.3%), Serbia (10.3%), Ujerumani (7.5%), Slovakia (5.8%), Bulgaria (5.2%), Bosnia na Herzegovina (4.8%), Kroatia (4.5%), Ukraine (3.8%), Ucheki (2.6%), Slovenia (2.2%), Moldova (1.7%), Uswisi (0.32%), Italia (0.15%), Poland (0.09%), Albania (0.03%) |
Urefu | 2,857 km |
Kimo cha chanzo | 1,087 m |
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | 6,500 m³/s |
Eneo la beseni (km²) | 801,463 km² |
Danubi ni mto mrefu wa pili katika Ulaya baada ya Volga.
Jina lina asili katika lugha za Kislanovi na kumaanisha kiasili "mto". Mto huu unapita katika nchi nyingi na majina yake ni Donau (Kijerumani), Dunărea (Kiromania), Dunav (Kikroatia na Kiserbia), Duna (Kihungaria) na Dunaj kwa Kislovakia.
Chanzo na mwendo
[hariri | hariri chanzo]Danubi inaanza Ujerumani ambako mito midogo ya Brigach na Breg inakutana karibu na mji Donaueschingen katika eneo la Msitu Mweusi. Danubi inaishia Romania katika delta yake kwenye Bahari Nyeusi.
Mto wa nchi kumi
[hariri | hariri chanzo]Danubi ni mto wa nchi kumi. Kwenye 1070 km (37 %) za mwendo wake mto ni mpaka wa nchi fulani. Mto haupiti hata kidogo ndani ya Kroatia, Bulgaria, Ukraine na Moldova lakini ni mstari wa mpaka wa nchi hizi zinagusana na Danubi tu ukingoni wa mto upande mmoja. Inapita katika nchi zifuatazo au kugusa mipaka yao:
Kilomita za mto nchini au mpakani |
Ukingo wa mto upande wa kulia |
Kingo zote mbili | Ukingo wa mto upande wa kushoto | ||||
Nchi - jina la mto nchini | km | % | km | % | km | % | |
Ujerumani - Donau | 687,00 | 658,6 | 23 | 658,6 | 36 | 687,0 | 24 |
Austria - Donau | 357,50 | 357,5 | 12 | 321,5 | 18 | 321,5 | 11 |
Slovakia - Dunaj tamka: dunay |
172,06 | 22,5 | 1 | 22,5 | 1 | 172,1 | 6 |
Hungaria - Duna | 417,20 | 417,2 | 14 | 275,2 | 15 | 275,2 | 10 |
Kroatia - Dunav | 137,50 | 137,5 | 5 | 0,0 | 0 | 0,0 | 0 |
Serbia - Дунав / Dunav | 587,35 | 449,9 | 16 | 220,5 | 12 | 358,0 | 12 |
Romania - Dunăre | 1075,00 | 374,1 | 13 | 319,6 | 18 | 1020,5 | 35 |
Bulgaria - Дунав (Dunav) | 471,55 | 471,6 | 16 | 0,0 | 0 | 0,0 | 0 |
Moldova - Dunare | 0,57 | 0,0 | 0 | 0,0 | 0 | 0,6 | 0 |
Ukraine - Дунай (Dunay) | 53,94 | 0,0 | 0 | 0,0 | 0 | 53,9 | 2 |
Namba za asilimia zinahusu urefu wa mto wote na sehemu ya kila nchi (Rejeo: Kamati ya kimatifa ya Danubi, Budapest, Januari 2000-Machi 2004)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Meli za mtoni kwenye Danubi
-
Mfereji kati ya Danubi na Bahari Nyeusi
-
Danubi mjini Visegrád, Hungaria
-
Daraja la Danubi mjini Bratislava (Slovakia)
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Danubi (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |