Nenda kwa yaliyomo

Basilio Pompili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Basilio Pompili

Basilio Pompili (16 Aprili 18585 Mei 1931) alikuwa askofu mkuu wa Kanisa Katoliki kutoka Italia, aliyehudumu kama Makamu wa Papa kwa Kanisa la Roma kuanzia mwaka 1913 hadi kifo chake. Alipandishwa hadhi kuwa kardinali mwaka 1911.

Basilio Pompili alizaliwa Spoleto na alisoma katika Seminari ya Kipapa ya Roma kabla ya kupewa daraja ya upadre tarehe 5 Desemba 1886. Baada ya hapo, alifanya kazi ya kichungaji mjini Roma kuanzia mwaka 1888 hadi 1904. Katika kipindi hicho, Pompili aliteuliwa kuwa msikilizaji wa Baraza Takatifu la Mtaguso mwaka 1891, afisa wa Kitubio cha Kipapa mwaka 1896, na kiongozi msaidizi wa Baraza la Mtaguso tarehe 16 Machi 1898. Alipewa cheo cha protonotari wa kitume tarehe 18 Desemba 1899, na kuteuliwa kuwa msikilizaji wa Mahakama ya Rota ya Roma tarehe 18 Julai 1904. Wakati wa utumishi wake katika Rota ya Roma, Pompili alishiriki katika kesi ya sita ya kutengua ndoa ya Paul Ernest Boniface na Anna Gould.[1]

  1. "Courts". Time. 13 April 1925.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.