Bahari ya Arafura
Mandhari
9°30′S 135°0′E / 9.500°S 135.000°E
Bahari ya Arafura (kwa Kiingereza: Arafura Sea) inapatikana katika magharibi ya Bahari Pasifiki, kati ya Australia na Guinea Mpya.
Urefu wake ni kilomita 1,290 ikiwa na upana wa km 560. Kina cha maji si kirefu, kwa kawaida mita 50 hadi 80 pekee. Kina huongezeka upande wa magharibi.
Wakati wa enzi ya barafu iliyopita sehemu kubwa ya maji duniani ilikuwa imeganda kuwa barafu na hivyo usawa wa bahari ulikuwa duni. Wakati ule sehemu ya Arafura ulikuwa nchi kavu ambako watu wa kwanza waliweza kupita na kufika Australia kutoka Asia.
Makala hii kuhusu maeneo ya Australia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Arafura kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |