Nenda kwa yaliyomo

Atlas (mitholojia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa matumizi tofauti ya jina hili tazama Atlas (maana)

Atlas akibeba anga (sanamu ya Kiroma, karne ya pili BK)

Atlas (kutoka Kigiriki: Ἄτλας atlas) alikuwa mungu mmojawapo katika dini ya Ugiriki ya Kale aliyehesabiwa katika nasaba ya miungu ya Watitani.

Katika masimulizi ya Wagiriki alikuwa mwana wa Iapetos na Asia, binti Okeanos. Baada ya vita ya Watitani dhidi ya miungu Waolimpo Atlas alipewa adhabu ya kusimama kwenye kona ya magharibi ya Dunia na kumbeba Urano, yaani anga. Hivyo Zeu alitaka kuzuia Urano (anga) kukutana tena na Gaia (Dunia, ardhi) na kuzaa.

Ilhali Mlango wa Gibraltar (kati ya Afrika Kaskazini na Ulaya) ulikuwa mwisho wa Dunia iliyojulikana na Wagiriki wa Kale, mitholojia ya Atlas iliunganishwa na milima mirefu kaskazini mwa Moroko ya leo. Milima hiyo hadi leo huitwa milima ya Atlas.

Tangu kuunganishwa na Afrika ya Kaskazini-Magharibi, Atlas aliendelea katika masimulizi mengine ya Waroma wa Kale kuwa mfalme wa Mauretania aliyesifiwa kwa elimu na hekima yake.

Mwanajiografia Gerardus Mercator alikusanya ramani nyingi katika kitabu kimoja akaita mkusanyo huo kwa heshima ya huyo mfalme "Atlas" na tangu hapo jina la atlasi linapatikana hadi leo kwa kitabu cha ramani.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.