Nenda kwa yaliyomo

Antiokia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Antiokia leo.
Antiokia

Antiokia ya Siria (kwa Kituruki: Antakya) ni mji wa Uturuki, kwenye mto Oronte, karibu na Bahari ya Mediteranea na mipaka ya Syria.

Ni makao makuu ya wilaya ya Hatay na wakazi wake ni 139.000 (2001); ni muhimu sana kwa akiolojia.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Zamani za ustaarabu wa Kigiriki ulikuwa jiji pamoja na Roma na Aleksandria, muhimu kwa biashara na elimu, lakini baada ya kuangamizwa na tetemeko la ardhi mwaka 525 B.K. na kutekwa na Waajemi mwaka 540 ulirudi nyuma sana.

Katika Biblia na historia ya Kanisa

[hariri | hariri chanzo]

Katika historia ya Kanisa umuhimu wa mji huo ulisisitizwa kwanza na Mwinjili Luka katika Matendo ya Mitume, alipoonyesha kwamba ni huko Antiokia kwamba wafuasi wa Yesu Kristo walianza kubatiza watu wengi wasio Wayahudi bila ya kudai wafuate Torati.

Hivyo Kanisa lilionekana wazi si madhehebu ya Uyahudi, bali dini mpya. Ndiyo sababu watu waliwatungia jina jipya, "Wakristo" (watu wa Kristo). Sababu nyengine ni tabia zao, matendo yao na hotuba zao zilikuwa kama za Kristo. Ilitumika kiasili na watu wasiookoka wa Antiokia kama jina la kimajazi (utani) ili kuwadhihaki wakristo hao. Ina maana sawa na “Kuwa mmoja wa kundi la kristo” au “mfuasi wa kristo,” ambayo imefanana na tafsiri ya Neno hili katika kamusi ya Webster.

Baadaye, Antiokia ukawa kituo kikuu cha kuendea umisionari kwa Mtume Paulo na Mtume Barnaba.

Baadaye tena, Antiokia ukawa kituo kikuu kimojawapo cha teolojia, kilichoshindana na Aleksandria. Tunda lake bora ni Yohane Krisostomo.

Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Antiokia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.