Alan Paton
Alan Stewart Paton (11 Januari 1903 – 12 Aprili 1988) alikuwa mwandishi wa nchi ya Afrika Kusini na mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Familia
[hariri | hariri chanzo]Paton alizaliwa katika eneo la Pietermaritzburg, Mkoa wa Natal ( ambao sasa unajulikana kama KwaZulu-Natal), babake alikuwa mtumishi wa kiserikali.[1] Baada ya kumaliza masomo yake katika Maritzburg College, alipata Shahada yake ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Natal [1] katika mji wake wa nyumbani, baada ya hapo alipata shahada ndogo ya ualimu. Baada ya kumaliza masomo yake, Paton alifanya kazi kama mwalimu, kwanza katika Shule ya Msingi ya Ixopo, na baadaye katika Shule ya Upili ya Pietermaritzburg[1] Alipokuwa katika shule ya Ixopo alikutana na Dorrie Francis Lusted.[1] Alimuoa Dorrie mnamo mwaka wa 1928 na walibaki pamoja hadi Dorrie alipokufa kutokana na ugonjwa wa shida ya kupumua mnamo mwaka wa 1967.[1] Maisha yao pamoja yanaelezewa katika kitabu kingine Kontakion Kwa Wewe Uliyeenda, iliyochapishwa mnamo mwaka wa 1969. Paton na katibu wake, Anne Hopkins, walifanya ndoa mwaka uo huo.[1]
Maisha mapema ya kitaaluma
[hariri | hariri chanzo]Alisimamia Shule ya Marekebisho ya Diepkloof ya (Waafrika) waliovunja sheria kati ya mwaka wa 1935 na 1948, ambapo alianzisha mabadiliko yaliyokuwa ya kuboresha maisha ya Waafrika gerezani.[1] Muhimu sana kati ya mabadiliko haya ilikuwa sera ya mabweni wazi, sera ya ruhusa ya kazi na sera ya kutembelea nyumbani. Mwanzoni, wavulana walipewa makazi katika mabweni yaliyofungwa. Lakini wakati walipojionyesha kuwa waaminifu, walihamishwa hadi mabweni yaliyokuwa wazi katika ardhi ya shule hiyo. Wavulana walioonyesha kiwango kikubwa cha uaminifu waliruhusiwa kufanya kazi nje ya ardhi ya shule. Wakati mwingine, wavulana waliruhusiwa hata kukaa nje ya ardhi ya shule huku wakilindwa na familia yao. Ni jambo lisilokuwa la kawaida kuwa wavulana wachache kuliko 1% walikosa kurudi, kutoka idadi ya wavulana 10,000 waliopewa ruhusa ya kwenda nyumbani wakati Paton alipokuwa msimamizi wa Shule ya Diepkloof ndio waliovunja imani yao kwa kukosa kurudi.
Paton alijitolea wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, lakini alikataliwa. Baada ya vita alitembea, kwa kutumia pesa zake, kutazama magereza Duniani kote. Alitembelea Sandinavia, Uingereza, Bara Ulaya na Marekani. Wakati alipokuwa nchini Norwei, aliandika riwaya yake marufu Lia, Nchi Nayoipenda, ambayo aliimaliza wakati wa safari yake, huku akiikamilisha siku kabla ya Krisimasi mjini San Francisco mnamo mwaka wa 1946.[1] Pale, alikutana na Aubrey na Marigold Burns, ambao walisoma rasimu ya kitabu chake na wakapata mchapishaji wa kukichapisha. Mhariri Maxwell Perkins, maarufu kwa kuhariri riwaya za Ernest Hemingway na Thomas Wolfe, aliongoza riwaya ya kwanza ya Paton ilipokuwa ikichapshwa na wachapioshaji wa Scribner.
Upinzani dhidi ya ubaguzi wa rangi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo mwaka wa 1948, miezi mine baada ya kuchapishwa kwa Lia, Nchi Inayopendwa, chama cha utengano cha Kimataifa kilichukua mamalaka nchini Afrika Kusini. Mnamo mwaka wa 1953 Paton alianzisha chama cha Uhuru Cha Afrika Kusini, ambacho kilipambana na sheria za ubaguzi wa rangi zilizoanzishwa na Chama cha Kimataifa. Libaki kama rais wa chama hicho hadi wakati kilipolazimishwa kuvunjwa na serikali ya ubaguzi katika miaka ya 1960, kwa sababu wanachama wake walikuwa weusi na weupe. Paton alikuwa rafuiki yake Bernard Friedman, mwanzilishi wa Chama cha Maendeleo (Afrika Kusini) [2]. Rafiki ya Paton aliyekuwa mwandishi Laurens van der Post, aliyekuwa amehamia Uingereza katika miaka ya 1930, alikisaidia chama kwa njia nyingi.
Van der Post alijua kuwa Majeshi ya Kijasusi ya Afrika Kusini yalijua kuwa alikuwa akimlipa fedha Paton, lakini haingeweza kukomesha shughuli hiyo kupitia njia halali za kisheria. Paton mwenyewe alifahamika kwa upinzani wake wa amani dhidi ya mfumo wa ubaguzi wa rangi, kama tu watu wengi katika chama chake, ingawa wachache walitumia njia ya moja kwa moja, ya vurugu. Kutokana na hayo, chama kilitazamwa kama mtenda mbaya kwa sababu ya matukio haya. Pasipoti ya Paton ilinyakuliwa aliporudi kutoka New York mnamo mwaka wa 1960, ambapo alikuwa amepewa Tuzo la Kila Mwaka la Utetezi wa Uhuru. Pasipoti hiyo ilirudishwa tuu baada ya miaka kumi. Paton alistaafu katika eneo la mlima wa Botha, ambapo aliishi hadi kifop chake. Anakumbukwa katika eno la Uhuru la Shirika la Uhuru la Kimataifa.
Maandiko mengine
[hariri | hariri chanzo]Riwaya za pili na za tatu za Paton, Phalarope anayechelewa sana (1953) na Ah, lakini Nchi yako ni Nzuri (1981), na hadithi zake fupi, Hadithi Kutoka Eneo Lenye Shida (1961), zote zinahusu na mada ile ile ya ubaguzi wa rangi zilizokuwa katika kitabu cha kwanza cha mwandishi huyo. Ah, lakini nchi yako ni nzuri ilikuwa na msingi wake katika hadithi za maisha, barua, hotuba, habari na rekodi za kesi za kisheria, na wahusika wa kubuni na wa kweli kama vile Albert Luthuli na Hendrik Verwoerd. Riwaya yenyewe ilikuwa ubunifu wa kihistoria, iliyotoa maelezo yenye ufasaha kuhusu harakati za upinzani nchini Afrika Kusini wakati wa miaka ya 1960. "Paton anajaribu kuwapa wahusika wake ubinadamu ambao hautarajiwi kutoka kwao. Katika riwaya hii, kwa mfano, tunakutana na Muafrikana mkaidi anayekiuka Sheria dhidi ya Uovu. Kuna Waafrikana wengine pia wanaaongozwa na na nia yao na si sheria, na kanuni zinazotolewa na bunge lisilokuwa na uso na lenye kushikilia mtazamo mmoja tu." (kutoka kitabu cha Waandishi wa Kiafrika wa baada ya Enzi ya Kikoloni,kilichohaririwa na Pushipa Naidu Parekh na Siga Fatima Jagne, 1998)
Paton alikuwa mwandishi wa insha nyingi, maudhui yake tena yakiwa kuhusu watui wa rangi mbalimbali na siasa nchini Afrika Kusini. Katika riwaya ya Okoa Nchi Inayopendwa Paton anatumia mada maarufu ya riwaya yake ya kwanza lakini anatumia sauti ya aadilifu katika kitabu chote huku akiwajadili watu wengi maarufu na maswala katika pande zote mbili za harakati za upinzani dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Dhehebu lake la Kianglikana lilikuwa jambo linguine lililochangia maisha yake na maandishi yake, kama inayoonekana kutoka kwa jina la kitabu Chombo cha Amani Yako. Paton aliandika vitabu viwili kuhusu maisha yake: Kuelekea Mlimani kinachohusu maisha ya Paton huku yakielekea (na hata kuhusisha) uchapishaji wa Lia, Nchi Inayopendwa (tukio lililobadilisha maisha yake) huku Safari Ikiendeleshwa inaanza kuhadithia kuanzia wakati huo kuendelea. Aliandika vitabu viwili kuhusu maisha ya watu wengine pia. Rafiki yake Jan Hendrik Hofmeyr alipewa heshima katika kitabu kilichoitwa Hofmeyr kama tu rafiki mwingine, Geoffrey Clayton, katika Ubaguzi wa Rangi na Kasisi. Mbinu nyingine ya uandishi iliyochukua wakati wake mwingi maishani mwake ilikuwa ushairi; mwandishi wa vitabu kuhusu maisha ya watu Peter Alexander anajumuisha mengi ya mashairi haya katika kitabu chake kuhusu maisha ya Alan Paton.
Vitabu vilivyochapishwa hivi karibuni kuhusu maandiko ya Paton ni vitabu kuhusu safari -- Mji Uliopotea wa Kalahari (2006); na baadhi ya maandiko yake mafupi -- Shujaa wa Barabara ya Currie.
Maisha ya Kibinafasi
[hariri | hariri chanzo]Paton alikuwa Mkristo wa kujitolea. Imani yake ni bayana katika vitabu alivyoviandika, Lia Nchi Inayopendwa, ikiwa ni mfano mmoja. Paton alikuwa na elimu nyingi, na anaaminika kuwa mmoja wa watu wenye kubarikiwa na akili nyingi Barani Afrika. Lengo lake la kibinafsi lilikuwa, "Afrika Kusini lazima iokolewe mtu mmoja kwa wakati."
Baadhi ya Vitabu Vyake
[hariri | hariri chanzo]- Lia, Nchi Nayoipenda, 1948 - filamu 1951, iliongozwa na Zoltan Korda
- Kupotea Angani 1950 (pamoja na Maxwell Anderson – ilifanywa kuwa wimbo na Kurt Weill)
- Phalarope Aliyechelewa Sana, 1953
- Ardhi ya Watu wa Afrika Kusini, 1955
- Afrika Kusini Ikibadilika, 1956
- Debbie Nenda Nyumbani, 1960
- Hadithi Kutoka Nchi Yenye Shida, 1961
- Hofmeyer, 1964
- Spono, 1965 (pamoja na Krishna Shah)
- Mtazamo wa Mbali, 1967
- Kifaa cha Amani Yako, 1968
- Kontakio, Kwa Wewe Uliyeenda, 1969 (pia: Kwa Wewe Uliyeenda)
- Historia ya Kesi ya Pinky, 1972
- Ubaguzi wa Rangi na Kasisi: Maisha na Matukio ya Geoffrey Clayton, Kasisi wa Cape Town, 1973
- Kubisha Mlangoni, 1975
- Kuelekea Mlimani, 1980
- Ah, lakini Nchi Yako ni Nzuri, 1981
- Safari Ikiendeleshwa: Hadithi ya Maisha, 1988
- Okoa Nchi Inayopendwa, 1989
- Shujaa wa Barabara ya Currie: hadithi ndogo kamili, 2008 [1]
Lia, Nchi Inayopendwa imefanywa kuwa filamu mara mbili (mwaka wa 1951 na 1995) na ilikuwa msingi wa Mchezo wenye Wimbo ulioitwa Kupotea Angani (iliigizwa na Maxwell Anderson]], muziki uliundwa na Kurt Weill). Tuzo la Alan Paton la Kila mwaka hutolewa ili kumkumbuka.
Angalia pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The Alan Paton Centre & Struggle Archives Archived 30 Agosti 2009 at the Wayback Machine.
- Alan Paton — A short biography and bibliography Archived 3 Aprili 2005 at the Wayback Machine.
- Cry the Beloved Country (1951) at the Internet Movie Database
- Cry the Beloved Country (1995) at the Internet Movie Database
- http://www.mg.co.za/article/2005-11-14-a-mixture-of-ice-and-fulfilled-desire