Aachen
Aachen | |
Mahali pa Aachen katika Ujerumani |
|
Majiranukta: 50°46′31″N 06°04′58″E / 50.77528°N 6.08278°E | |
Nchi | Ujerumani |
---|---|
Jimbo | Rhine Kaskazini-Westfalia |
Idadi ya wakazi (2009) | |
- Wakazi kwa ujumla | 258,380 |
Tovuti: http://www.aachen.de/ |
Aachen (tamka: akhen) ni jiji la nchini Ujerumani ambalo lipo katika jimbo la Rhine Kaskazini-Westfalia.
Mji huo una wakazi wapatao 260,000 wanaoishi huko na unajulikana kwa kuwa na chuo kikuu cha Rheinisch-Westfälisch Technische Hochschule (RWTH) na kuwa na historia nzuri ya kuanzia mwanzoni mwa Karne za Kati.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Chanzo cha Aachen kilikuwa chemchemi za maji moto zilizotumiwa na watu kama tiba ya maradhi mbalimbali.
Waroma wa Kale walijenga huko bafu kwa jina la Aquis-Granum maana yake maji ya mungu wa tiba aliyeitwa Granus.
Karolo Mkuu alipenda kuja huko akaagiza kujengwa kwa mji kamili akaufanya kuwa mji mkuu wake akaupamba kwa kanisa mashuhuri mnamo mwaka 786 BK. Kanisa hili leo hii limeshapokewa katika orodha ya urithi wa dunia.
Tangu mwaka 1972, Aachen imekuwa moja kati ya sehemu za Mkoa wa Kiserikali wa Cologne.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Aachen kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |