Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Coolsam726

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 08:00, 22 Agosti 2015 na Coolsam726 (majadiliano | michango) (Nimetafsiri maelezo ya utangulizi kwa lugha ya Kiswahili.)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)

Huu ni ukurasa wa Sam Maosa, mtumiaji wa Wikipidia ya Kiswahili tangu mwaka wa 2009. Yeye hujishughulisha hasa na kutafsiri makala ya wikipidia kutoka Kiingereza hadi Kiswahili. Maosa amehitimu kutoka katika Chuo kikuu cha Jomo Kenyatta (Kenya) akiwa na shahada katika Uhandisi wa Elektroniki na Tarakilishi. Ufuatao ni ujumbe wake wa awali:

PICHA YANGU
KUNIHUSU:

Bendera ya Kenya Kenya

KWC Mtumiaji huyu ni mwanafunzi katika JKUAT.
KWC Mtumiaji huyu ni mshiriki katika Shindano la Wikipedia ya Kiswahili la 2009.   (Submissions)


sw Mtumiaji huyu lugha mama yake ni Kiswahili.
en-3 This user is able to contribute with an advanced level of English.
es-1 Este usuario puede contribuir con un nivel básico de español.
fr-0 Cet utilisateur ne comprend pas le français, ou seulement avec des difficultés notables.

Ushiriki wangu katika Shindano la Wikipedia ya Kiswahili lililothaminiwa na Google umeniinua kwa njia nyingi:

  1. Nimeyajua mengi kuhusu lugha ya wiki markup na sasa ninaweza kutunga makala ya kumezewa mate na wengi.
  1. Nimejifunza kuchukua wakati wangu na kustahimili katika kazi yoyote ile, kwani kazi hii haikuwa rahisi. Ilihitaji moyo wa kujitolea, kishujaa na wa kutoghairi.
  1. Nimejifunza kuushirikiana na wenzangu katika jambo lolote lile. Funzo hili nimelipata kupitia kundi la nyarafa katika google lililoundwa kwa ajili ya mawasiliano kati ya wanawikipedia katika shindano hili.
  1. Kujua kwamba makala yangu inasaidia watu wengi wa Afrika Mashariki wanaohitaji ujumbe husika kwa kiswahili hunipa faraja kubwa.

Shukrani Zangu

[hariri | hariri chanzo]

Shukrani za dhati ziwaendee wadhamini wa Shindano hili, Google na Wikipedia. Shukrani kwa Watuza alama ambao nilikaa nikiwatazama wakiwa kwa mtandao karibu masaa ishirini na manne wakijaribu kukosoa na kuzituza makala zetu. Hongera sana kwani si kazi rahisi.

Kwa washiriki wote, asante sana kwa kushirikiana katika kuunda makala na kufafanua istilahi tofauti tofauti kwa wengine wasiokuwa na ujuzi mwingi kwani viwango vya ujuzi haviwezi kulingana.

Shukrani zangu pia ziiendee familia yangu kwa moyo mlionipa na pia kwa uthamuni wenu wa kifedha, hasa kwa kutumia mtandao. Shukrani kwa kakangu kwa kuniruhusu nitumie tarakilishi yako ya Kazi. Kwa marafiki zangu wote walionipa motisha, kuanzia wanafunzi wenzangu wa JKUAT na Vyuo vingine, hadi wale tunnaokutana kwa Tovuti, nyinyi ni wa thamani.

Juu ya hao wote, sina budi hata kidogo kumshukuru Mungu kwa kunijalia na kipawa na moyo huu, na pia kwa afya nzuri. Nisingeweza lolote bila yeye.

Maazimio

[hariri | hariri chanzo]

Kama shukrani kwa ujuzi na hati niliyoipata kupitia kwa shindan hili, ningependa kuendelea kuikuza Wikipedia ya Kiswahili kwa kukabidhi makala zaidi hata baada ya shindano hili.

Shirika la Google hunitia changamoto sana. Ni ndoto yangu kuwa siku moja baada ya masomo yangu ya Uhandisi wa Tarakilishi na Elektroniki, nitapata nafasi ya kuhudumu huko.

Tafadhali wasiliana nami kwa mengi zaidi katika sanduku langu la MAJADILIANO.