Nenda kwa yaliyomo

Albano Roe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 15:07, 13 Julai 2024 na InternetArchiveBot (majadiliano | michango) (Rescuing 1 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.9.5)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Mt. Albano akishika karata alizozitumia katika utume wake kama mfungwa.

Albano Roe, O.S.B. (Bury St. Edmunds, Suffolk, Uingereza, 20 Julai 1583Tyburn, London, 21 Januari 1642) alikuwa Mkristo wa Kanisa la Anglikana kabla hajajiunga na Kanisa Katoliki pamoja na ndugu yake James.

Baada ya kuhamia Ufaransa, aliingia seminari (1607) kwa kengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali, lakini alifukuzwa kwa tabia yake (1610). Baadaye alijiunga na monasteri ya Wabenedikto (1613) na kupewa daraja ya upadri (1615).

Hapo alirudi London lakini alifukuzwa baada ya muda mfupi. Alirudi tena mwaka 1618 akafungwa hadi 1623. Miaka miwili baadaye akarudi tena akafungwa kwa miaka 17, lakini gereza halikuwa na nidhamu kali, hivyo akaweza kufanya utume wake mchana na kurudi kulala jela usiku.

Mwaka 1641 alihamishiwa gereza lingine alipokataa kuasi na kwa ajili hiyo mwaka uliofuata aliuawa kwa kunyongwa chini ya sheria.

Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39.

Sikukuu yake ni tarehe 21 Januari[1].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.