Alama ya barabarani
Alama ya barabarani ni alama inayowekwa kwenye nguzo kando ya barabara ili kutoa habari, onyo au elekezo kwa watu wanaopita hapo kwa vyombo vya usafiri au kwa miguu.
Alama ya barabarani hutumia picha au matini mafupi ya neno moja au maneno machache kwa madereva au watumiaji wengine wa barabara.
Alama hizo huainishwa hivi:
- alama za onyo au tahadhari zinazotoa habari za hatari katika sehemu ya barabara inayofuata, kama vile kuruba kwenye mwendo wa barabara, uwezekano wa wanyama kukata njia, mitelemko, upepo mkali kwenye njia, sehemu nyembamba ya njia mbele (kama daraja). Alama hizo huwa kwa umbo la pembetatu.
- alama za amri, mara nyingi za kukataza, kama vile kutoingia barabara, kutopiga kona upande fulani, kutozidi kasi ya kiwango fulani. Alama hizo hutumia umbo la mviringo.
- alama za maelekezo na taarifa. Alama hizo hutoa maelekezo juu ya utumiaji bora wa barabara au uelekeo, na huwa katika umbo la pembe nne na mara nyingi kwa rangi ya buluu, kijani au nyekundu.
- alama za michoro ya sakafuni zinazodokeza njia maalum, mahali pa kusimama, nafasi ya waenda kwa miguu.
Kwa kawaida alama za barabarani hutumia umbo sanifu na kufuata utaratibu wa kisheria zikiwa pia na nguvu ya kisheria. Wakati mwingine kuna pia alama zilizotengenezwa na kusimamishwa kimahali ambazo zinaonekana tofauti.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alama ya barabarani kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |