Hangul ni alfabeti ya Kikorea. Iliundwa mnamo mwaka 1443 kwa amri ya mfalme Sejong alliyeona ya kwamba maandishi ya Kichina haifai kwa lugha ya Korea. Nchini Korea ya Kaskazini Hangul huitwa Chosŏn'gŭl.

Hangul

Hangul ina alama za kimsingi 24 kwa konsonanti na vokali. Lakini alama hizi haziandikwi mfululizo kama kaika alfabeti ya Kilatinilakini zinapangwa katika alama za herufi za silabi moja kama 한 han.

Hiyo 한 han inaonekana kama alama 1 lakini ali halisi ni herufi tatu: ㅎ h, ㅏ a na ㄴ n. Kila alama kwa silabi inashika ndani yake herufi 2 hadi 6. Alama za silab zinaweza kuandikwa kama mstari kuanzia kushoto kwenda kulia au kutoka juu kwenda chini, kama maandishi ya Kichina.