Papers by Adika, Stanley Kevogo
Research on Humanities and Social Sciences, 2014
Research on Humanities and Social Sciences, 2015
Kioo cha Lugha, 2015
Ulimwengu wa sasa wa utandawazi umesababisha kuzagaa kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawa... more Ulimwengu wa sasa wa utandawazi umesababisha kuzagaa kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hususani kompyuta na vitumi vyake. Kwa hali hiyo, maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesababisha kuenea kwa lugha zinazotumika kwa wingi katika teknolojia hiyo kama vile Kiingereza na Kifaransa na kudumazwa kwa lugha za Kiafrika zinazotumiwa kwa nadra mno. Uwezo wa kutumia media na vitumi vipya vya teknolojia hii kwa ubunifu na uhakiki aghalabu hutegemea umilisi wake. Umilisi wa kidijitali nao ni zao la mafunzo kupitia lugha zoefu ambayo humpa mwanafunzi fursa ya kushiriki kikamilifu. Makala hii ni sehemu ya matokeo ya uchunguzi mdogo uliofanywa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania kuonesha ufaafu wa Kiswahili kama lugha rasmi ya kufundishia somo la TEHAMA katika shule za msingi. Matumizi ya Kiswahili kufundishia stadi za msingi za TEHAMA ni hatua ya mwanzo kuelekea kwenye matumizi ya lugha ya Kiswahili kutolea mafunzo ya kiufundi. Aidha, tunatathmini manufaa na changamoto zinazokabili matumizi ya Kiswahili kama lugha ya TEHAMA.
Research on Humanities and Social Sciences, 2013
Jarida la Mnyampala, 2020
Maendendeleo katika taaluma ya leksikografia yamepelekea kuwepo kwa idadi kubwa ya kamusi za isti... more Maendendeleo katika taaluma ya leksikografia yamepelekea kuwepo kwa idadi kubwa ya kamusi za istilahi za Kiswahili katika nyanja za taaluma mbalimbali. Hata hivyo, licha ya maendeleo hayo, hakuna kamusi kamilifu isiyo na upungufu wa aina fulani. Kwa kutumia mbinu za utafiti wa maktabani, makala haya yanachunguza na kuchanganua mikakati na mbinu ambazo zimekuwa zikitumika katika utungaji wa kamusi za kiistilahi za Kiswahili. Data inayotumika ni sampuli ya istilahi za kompyuta zilizoorodheshwa kama vidahizo katika Kamusi Sanifu ya Kompyuta (Kiputiputi, 2011). Azma yetu ni kubainisha mbinu zinazofaa zaidi katika utungaji kamusi za istilahi za Kiswahili zitakazokidhi mahitaji ya lugha hiyo katika kipindi hiki na siku za usoni. Hoja kuu ya makala haya ni kwamba kuegemea zaidi kwenye mbinu za tafsiri na zile za kileksikografia badala ya zile za kiteminografia katika utungaji wa kamusi za istilahi za Kiswahili kumetinga ufanisi katika sayansi na sanaa hiyo.
Kioo cha Lugha, 2017
Ulimwengu wa sasa wa utandawazi umesababisha kuzagaa kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawa... more Ulimwengu wa sasa wa utandawazi umesababisha kuzagaa kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), hususani kompyuta na vitumi vyake. Kwa hali hiyo, maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesababisha kuenea kwa lugha zinazotumika kwa wingi katika teknolojia hiyo kama vile Kiingereza na Kifaransa na kudumazwa kwa lugha za Kiafrika zinazotumiwa kwa nadra mno. Uwezo wa kutumia media na vitumi vipya vya teknolojia hii kwa ubunifu na uhakiki aghalabu hutegemea umilisi wake. Umilisi wa kidijitali nao ni zao la mafunzo kupitia lugha zoefu ambayo humpa mwanafunzi fursa ya kushiriki kikamilifu. Makala hii ni sehemu ya matokeo ya uchunguzi mdogo uliofanywa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania kuonesha ufaafu wa Kiswahili kama lugha rasmi ya kufundishia somo la TEHAMA katika shule za msingi. Matumizi ya Kiswahili kufundishia stadi za msingi za TEHAMA ni hatua ya mwanzo kuelekea kwenye matumizi ya lugha ya Kiswahili kutolea mafunzo ya kiufundi. Aidha, tunatathmini manufaa na changamoto zinazokabili matumizi ya Kiswahili kama lugha ya TEHAMA.
This study investigated language attitudes of secondary school learners of Somali descent toward ... more This study investigated language attitudes of secondary school learners of Somali descent toward Kiswahili and their patterns of language use in various domains in a multilingual context as evidenced in Garissa Town. The target population was secondary school students in public and private schools within Garissa town, Garissa County, Kenya. Field data was collected through questionnaires. A total of 100 respondents were involved in this study. This sample was obtained through simple random sampling technique. This study obtained quantitative data from respondents’ responses to guided questionnaires in order to determine their attitude towards Kiswahili. Data was analysed descriptively and by way of tables. The findings reveal that secondary school students within Garissa town have a positive attitude toward Kiswahili. Somali language is mainly spoken at home. English is mainly spoken at school while Kiswahili is used for intercultural and interethnic communication.
Keywords: Patterns of Language Use, Language Attitudes, Multilingualism, Kiswahili
Kiswahili, like all languages, is dynamic. It evolves to accommodate economic, scientific, techno... more Kiswahili, like all languages, is dynamic. It evolves to accommodate economic, scientific, technological and social changes. Such changes are evident in Kiswahili military terms. The changes can be traced back to the 16th century contacts with visitors from Asia and Europe to the East African Coast. The outcomes of these contacts were borrowed military terms which form relics of their impact on Kiswahili vocabulary. Moreover, with the advent of globalization and its attendant Information Communication Technologies (ICTs), Kiswahili has more contact with the outside world via English. Kiswahili has grown from describing rudimentary military strategies, processes and hardware to describing today’s highly sophisticated warfare. While such changes might appear inevitable, most of the military hardware is imported from Western countries. This paper therefore scrutinizes the non-institutionalised advancement of Kiswahili through the years to elaborate new military concepts such as terrorism (ugaidi), bomb (bomu), sniper (mdenguaji), nuclear weapons (silaha za kinyuklia), weapons of mass destruction (silaha za mauaji halaiki) and the linguistic strategies employed in creating such terms.
Key Words: Kiswahili, Military Terminology, Globalization, Vocabulary
Abstract
The role of language attitudes on language choice, development and policy in multilingua... more Abstract
The role of language attitudes on language choice, development and policy in multilingual societies cannot be over emphasized (Adegbija, 1994; Batibo, 2005). Monolingual speakers have only one attitude towards their language because they have no other languages to compare it with. However, where speakers are bilingual or multilingual; there is a tendency to develop different attitudes to each of the languages used. These attitudes, whether positive or negative, will normally depend on the degree of symbolic or socio-economic value manifested by each language. Tanzania, a multilingual country with over 128 languages and with a bilingual language policy in education is therefore a fertile ground for studies on language attitudes. In recent years, there have been concerted efforts by various stake holders to propagate growth and development of English in Tanzania. English has been lauded as the essential language which links Tanzania to the rest of the world through technology, commerce and administration. Against this backdrop, this study sought to investigate students’ attitudes towards Kiswahili so as to determine whether the shift to English had impacted students’ attitude formation towards Kiswahili. This survey comprised of 340 students sampled from six selected schools of Mtwara Urban and Mtwara Rural districts. Results show that most Tanzanian students have favourable attitudes towards Kiswahili and the language’s status among secondary school students has not diminished. Kiswahili remains the most preferred language of use in all major domains. This study proposes that the place and role of Kiswahili be further enhanced in the country by exploring its possible use as a medium of instruction at secondary school level. Further, the study proposes that local vernaculars, which face extinction due to language shift that has taken place, need drastic measures in order to preserve them.
Keywords: Multilingualism, Bilingual education, language attitudes, Kiswahili
Books by Adika, Stanley Kevogo
Katika Mukuthuria, M. na Kandagor, M. (wah.). Lugha ya Kiswahili: Utafiti na Maendeleo Yake. Dar es Salaam: TUKI na Chama cha Kiswahili cha Afrika Mashariki (CHAKAMA). Uk. 234-266., Aug 9, 2018
Maendeleo ya kasi yanayojiri ulimwenguni yameongeza haja ya mawasiliano miongoni mwa jamiilugha m... more Maendeleo ya kasi yanayojiri ulimwenguni yameongeza haja ya mawasiliano miongoni mwa jamiilugha mbalimbali. Maendeleo hayo yamepelekea matini za kiufundi kutafsiriwa haraka iwezeka-navyo. Kuongezeka kwa mahitaji ya tafsiri maalumu nako kunazalisha kiasi kikubwa cha istilahi. Hali hii inazua tatizo kwa mtafsiri, ambaye aghalabu huwa si mtaalamu wa uwanja unao-tafsiriwa. Kwa hivyo, ni muhali kupata tafsiri sahihi ya istilahi. Isitoshe, mtafsiri hupania kupunguza muda anaotumia kuhawilisha matini na kwa hali hiyo hawezi kupoteza muda mwingi kuchunguza visawe vya istilahi. Maelezo hayo yanasawiri vyema utendakazi wa wanahabari kwenye vyumba vingi vya habari. Wanahabari aghalabu hutekeleza wajibu wao kwa makataa fupi zilizobana kiasi kwamba, katika hali halisi, hawana muda kufanya uchanganuzi linganishi wa kina kuhusu istilahi wanazokumbana nazo. Ni katika usuli huo ambapo sura hii inachunguza mikakati inayotumiwa na wanahabari kukabiliana na changamoto za kiistilahi wanapowasilisha habari na ripoti kuhusu dhana mpya zisizopatikana katika mazingira, utamaduni na lugha ya Kiswahili. Istilahi zinazotumika kuwakilisha dhana mbalimbali za mfumo wa Serikali ya Ugatuzi zitachambuliwa. Azma kuu ni kubaini iwapo zinaafiki misingi na kanuni za uundaji istilahi katika lugha ya Kiswahili. Aidha, uchambuzi unafanywa kuthibitisha iwapo maumbo sanifu yanayohitajika ndiyo yanayotumika, yaani maumbo yanayoendana na kaida za othografia, uundaji istilahi na sheria za uandishi wa Kiswahili, na iwapo yanawakilisha maana inayowasilishwa na dhana zinazohusika. Kwa kuwa kila kukicha vyombo vya habari huwasilisha taarifa mbalimbali kuhusu mfumo wa Serikali ya Ugatuzi, istilahi nyingi ambazo zinaelezea uwanda huu zimepenyeza katika msamiati wa lugha ya kawaida. Watu hutumia istilahi zinazohusiana na mfumo wa ugatuzi katika lugha ya kawaida kana kwamba wanaelewa maana kamili ya istilahi hizo. Isitoshe, kuzagaa kwa vyombo vya habari vya kila sehemu huenda kunachangia kupenya kwa lugha ya kiufundi au lugha ya kitaalamu (Lugha kwa Matumizi Maalumu, LSP) kwenye lugha ya kikawaida (Lugha kwa Matumizi Jumla, LGP).
Katika Mukuthuria, M. na Kandagor, M. (wah.). Lugha ya Kiswahili: Utafiti na Maendeleo Yake. Dar es Salaam: TUKI na Chama cha Kiswahili cha Afrika Mashariki (CHAKAMA). Uk. 215-233., Aug 9, 2018
Blogu ni aina ya tovuti ambayo humwezesha mtumiaji wake kuweka matangazo mapya kila wakati. Matan... more Blogu ni aina ya tovuti ambayo humwezesha mtumiaji wake kuweka matangazo mapya kila wakati. Matangazo hayo ni yale yanayohusu taarifa, maoni, maelezo ya matukio, picha na hata video (DOTS, 2011). Neno blogu linatokana na kutoholewa kwa neno la Kiingereza ‘blog’ ambalo limeundwa kwa kuambatisha maneno ‘web’+‘log’ ili kuunda neno ‘weblog’. Istilahi ‘weblog’ ilibuniwa na John Barger mnamo 1997. Hata hivyo, istilahi hiyo ilifupishwa na Peter Merholz ikawa ‘blog’ mwaka 1999 (Blood, 2000). Taarifa kwenye blogu huonyeshwa kwa njia inayozingatia utaratibu maalum unaonyesha taarifa mpya kwanza kisha taarifa za zamani huja baadaye. Hii ina maana kuwa taarifa mpya huwa juu na ile ya zamani huwa sehemu ya mwisho ya blogu. Mara nyingi, huduma za blogu hutolewa bure japo kuna blogu chache ambazo zinamhitaji mtumiaji kulipia huduma hizo. Kimsingi, umaarufu wa blogu miongoni mwa watafiti na watumiaji wengine unatokana na wepesi wa kuzitumia (Ward, 2004). Isitoshe, taarifa kwenye blogu hupangwa kwa utaratibu mzuri unaozifanya ziwavutie wasomaji kwa vile zimeambatishwa na picha pamoja na vielelezo vingine vinavyozifafanua.
Blogu nyingi hutoa fursa kwa watumiaji kutoa maoni na michango yao kuhusu mada fulani. Baadhi ya blogu hufanya kazi kama shajara za kibinafsi za watumiaji ambao huandika matukio muhimu ya kisiasa, kiuchumi, kitaaluma na hata yale ya kidini. Blogu ya kawaida huwa na taarifa ya kimatini ambayo huambatana na picha na anwani za tovuti zinazomwelekeza mtumiaji kwenye tovuti zingine zinazohusiana na blogu husika. Isitoshe, tunaweza kupata kurasa mbalimbali za tovuti pamoja na vyombo tofauti vya habari vilivyo na taarifa inayohusiana na blogu inayohusika. Blogu huwa na uwezo wa kiutangamano unaotoa fursa kwa mtumiaji kushiriki kikamilifu kwenye midahalo kwa kutoa maoni yake kuhusu mada inayojadiliwa. Hali hiyo humwezesha kushirikiana na watumiaji wengine wa blogu. Uwezo huo wa kushirikiana huzifanya blogu kuwa kifaa muhimu cha kufundisha au kujifunza lugha kwa kundi kubwa la watu walio sehemu mbalimbali duniani (Ward, keshatajwa).
Kimuundo, blogu nyingi huwa za kimatini. Hii ina maana kwamba taarifa zinazopatikana kwenye blogu hizo ni za kimaandishi. Hata hivyo, kuna baadhi ya blogu zenye mwegemeo upande wa sanaa ya uchoraji yaani ‘art blog’, blogu za picha ‘photo blog’, blogu za video ‘vlog’, blogu za muziki ‘MP3 blog’, blogu za kielimu ‘edublog’ na blogu za kusikiliza habari ‘podcast’. Kwenye utafiti huu tutazingatia tu blogu za dini ya Kikristo zilizo za kimatini. Kwenye intaneti kuna vifaa vitatu ambavyo humwezesha mtafiti kukusanya blogu mbalimbali anazokusudia kuzitafiti. Vifaa hivyo ni pamoja na ‘Technorati’, ‘BlogScope’ na ‘Google blog search’. Utafiti huu ulizingatia kifaa cha ‘technorati’ kukusanya blogu za Kikristo zinazotumia Kiswahili katika eneo la Afrika Mashariki. Kifaa cha technorati kilitumiwa kwa sababu ya uwezo wake wa kutoa taarifa kuhusu blogu mbalimbali tofauti na ilivyo na vifaa hivyo vingine viwili. Kuna zaidi ya blogu ishirini zinazotumia Kiswahili kutoa ujumbe wa dini ya Kikristo Afrika Mashariki.
Blogu ni kifaa muhimu cha kueneza lugha duniani kutokana na uwezo wake wa kufanikisha utangamano baina ya wanablogu na watumiaji wengine wa blogu hizo kote duniani. Mwanablogu ni mwanahabari huru au mwandishi anayemiliki blogu; ndiye hasa anayeandika taarifa zinazotolewa kwenye blogu. Taarifa hizo husomwa na watumiaji wengine wa blogu ambao hutoa maoni, fikra, mawazo na mchango wao kuhusu mada ya mwanablogu. Kimsingi, blogu huwawezesha watumiaji kutoa maoni kuhusu taarifa zilizochapishwa kwenye blogu. Kwa hali hiyo, watumiaji wanao- jifunza lugha hupata fursa kujifunza lugha kimaandishi na vilevile kimazungumzo na kimasikizi kwa njia ya video. Watumiaji hupata fursa adimu kushiriki katika midahalo kwa kuuliza maswali, kutoa maoni na mchango wao kuhusu mada inayohusika. Mwitiko kutoka kwa watumiaji wenzao hutoa motisha kwa wale watumiaji wanaojifunza lugha kujiimarisha na kujimudu katika matumizi yao ya lugha. Isitoshe, utangamano kwenye blogu hujenga umoja miongoni mwa wanajumuiya wanaoshiriki katika mijadala na midahalo ambao hujihisi na kujiona kuwa sehemu ya jumuiya hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya www.dots.ecml (2011) utoaji wa makala kwenye blogu kila mara huimarisha umilisi wa kimaandishi wa watumiaji wa blogu wanojifunza lugha katika sehemu mbalimbali duniani. Hilo linatokana na ujasiri wa watumiaji blogu kujieleza wazi na kwa njia huru pasipo kujali makosa wala upungufu walionao. Isitoshe, watumiaji hao wa blogu huelewa kwamba wanaandikia hadhira pana iliyoenea kote duniani. Ufahamu huo hutoa changamoto kwao kujitahidi kutumia lugha ipaswavyo. Matumizi hayo ya lugha kwenye blogu tunayaona kuwa na manufaa ya kueneza lugha duniani. Hilo linatokana na watumiaji walioko katika maeneo mbalimbali duniani wanaojitahidi kufanya mazoezi ya kutumia lugha kimaandishi.
Sura hii inatalii michakato ya ukuzaji istilahi za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). ... more Sura hii inatalii michakato ya ukuzaji istilahi za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). Uundaji istilahi rasmi aghalabu hutekelezwa na mwanaistilahi mmoja, taasisi, chombo cha kisheria cha serikali au jopo la wataalamu wachache kwa ajili ya umma unaotumia lugha inayohusika. Watumiaji wa lugha huunda istilahi zao wenyewe kwa nadra mno. Kwa hali kama hiyo, baadhi ya istilahi unde hupingwa, kutoafikiwa au hata kukataliwa na watumiaji kwa sababu ama hawaelewi misingi iliyotumiwa kuziunda au hazioani na dhana zinazowakilishwa nazo. Baadhi ya watumiaji hupenda istilahi fulani kwa sababu ya upya au shani yake ilhali wengine hupenda istilahi za aina fulani kwa sababu ya mazoea tu. Hali hii imepelekea kuendelea kutoridhika miongoni mwa watumiaji wa lugha. Yamkini kuna uwezekano kuwa mchakato ambao ni bora zaidi ni ule usio rasmi na utokanao na watumiaji lugha wenyewe. Ni kutokana na usuli huu ambapo makala hii inachunguza mikakati isiyo rasmi ya ukuzaji wa istilahi za TEHAMA nchini Tanzania. Hili tunalifanya kwa kuchunguza uundaji wa istilahi usio rasmi miongoni mwa kampuni na watumiaji wa simu za mkononi. Tunabainisha vyanzo vya maneno mapya yanayotumika katika mawasiliano ya simu za mkononi. Tunahoji, Je, ipo tija iwapo watumiaji wa lugha watashirikishwa katika uundaji wa istilahi? Je kuna uhusiano na ulinganifu baina ya istilahi zinazoibuka katika mazingira haya?
Uploads