Pata taarifa kuu

DRC : Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya Corneille Nangaa kiongozi wa (AFC)

Mahakama ya Kijeshi ya Kinshasa/Gombe siku ya Alhamis iliendelea na uchunguzi wa kesi inayomhusisha Corneille Nangaa, aliyekuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) na kiongozi wa vuguvugu la kisiasa na kijeshi la Alliance Fleuve Congo (AFC), tawi la kisiasa la kundi la uasi wa M23, pamoja na washtakiwa wengine 24 wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa kivita, kushiriki katika harakati za uasi na uhaini.

Mahakama ya Kijeshi ya Kinshasa/Gombe siku ya Alhamis iliendelea na uchunguzi wa kesi inayomhusisha Corneille Nangaa.
Mahakama ya Kijeshi ya Kinshasa/Gombe siku ya Alhamis iliendelea na uchunguzi wa kesi inayomhusisha Corneille Nangaa. AFP/Luis Tato
Matangazo ya kibiashara

Washtakiwa watano kati ya waliokuwepo walisikilizwa wakati kesi hiyo iliovuta hisia za wengi ikiendelea kusikilizwa. Washukiwa wametoa ushuuhda wa shguhuli za AFC katika mataifa jirani hususan Rwanda na Uganda.

Mbele ya majaji Eric Nkuba Malembe ameeleza baada ya uundwaji wa AFC nchini Kenya, yeyé na Corneille Nangaa waliekea Uganda na kudhibitisha kuwa walipewa malazi katika Hoteli iliotolewa na mtoto wa rais wa Uganda jenerali Muhoozi Kainerugaba.

Corneille Nangaa aliwahi kuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI)
Corneille Nangaa aliwahi kuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) AFP - JOHN WESSELS

Mtuhumiwa Kangya Nyamachomi ameiambia mahakama kwamba alikutana na Corneille Nanga mjini Kigali wakiwepo watu wenye asili ya Rwanda na kwamba Corneille Nangaa alikuwa amekutana na wawakilishi kutoka Kivu kuwaomba wajiunge na shughuli za AFC.

Mtuhumiwa mwingine amethibitisha kuwa AFC inamakundi mawili wa kijeshi ambamo ni M23 katika Mkoa wa Kivu Kaskazini na Twirwaneho Kivu kusini, na kusisitiza kuwa lengo hasa la AFC sio tu kuuteka mji wa Goma bali ni kusonga mbele hadi Kinshasa na kuipindua serikali ya Felix Tshisekedi.

Makundi ya waasi yamekuwa yamekuwa yakitekeleza mashambulio dhidi ya raia wa mashariki ya DRC.
Makundi ya waasi yamekuwa yamekuwa yakitekeleza mashambulio dhidi ya raia wa mashariki ya DRC. AFP - ALEXIS HUGUET

Wakati hayo yakijiri, Marekani imetangaza kuwa imechukua vikwazo dhidi ya Corneille Nangaa, kiongozi wa Muungano wa (AFC) na baadhi ya washirika wake, akiwemo Bertrand Bisimwa wa M23 na Charles Sematama, kamanda na naibu kiongozi wa kijeshi wa Twirwaneho kundi lenye silaha linaloshirikiana na AFC katika jimbo la Kivu Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.