Pata taarifa kuu

Amnesty yashutumu 'ukandamizaji' wa wapinzani Mashariki mwa Libya

Katika ripoti yake, shirika la kimlataifa la haki za Binadamu la Amnesty International linashutumu Idara ya Usalama wa Ndani, ambayo iko chii ya mamlaka ya Jeshi la Taifa la Libya linaloongozwa na Marshal Khalifa Haftar, kuhusika na vifo vya watu walioko kizuizini, mauaji na watu kuwekwa kizuizini kiholela.

Raia wa Libya wakiwa nje ya ofisi ya jeshi huko Benghazi, mashariki mwa nchi hiyo.
Raia wa Libya wakiwa nje ya ofisi ya jeshi huko Benghazi, mashariki mwa nchi hiyo. AFP - MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Ikiongozwa na Osama al-Derssi, Idara ya Usalama wa Ndani, inayoelezewa na Amnesty kama "kundi lenye silaha", inawatia hofu wajosoaji na wapinzani, wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, wanaharakati, waandishi wa habari na wanablogu.

Kulingana na shirika hilo lisilo la kiserikali, makumi ya watu walikamatwa mashariki mwa Libya bila kibali na watu waliokuwa na silaha nzito. Watu hawa wananyimwa mawasiliano na familia zao au wanasheria, wanateswa na hawahukumiwi kamwe au kufikishwa mbele ya mamlaka ya mahakama ya kiraia.

"Ukiukwaji wa haki ya kuishi"

Watu wawili walifariki wakiwa kizuizini katika mazingira tatanishi huko Benghazi na Ajdabia. Hakuna uchunguzi huru umefanywa. Amnesty inataka kusimamishwa kazi kwa wale waliohusika na unyanyasaji huo na pia kufunguliwa kwa uchunguzi huru. Miongoni mwa waliokamatwa kiholela ni mwanablogu kutoka Sebha, Maryam Mansour el Werfalli. Mnamo mwezi Januari, alikosoa usimamizi wa uhaba wa gesi katika jiji lake.

Mfano mwingine, Sheikh Ali Mesbah abou Sbiha, mwenye umri wa miaka 77, mkuu wa baraza kuu la makabila ya Fezzan, anakosoa kukamatwa kiholela. Alipoachiliwa huru mwezi Juni mwaka jana, ilimbidi ahame nyumbani kwake baada ya kupokea vitisho.

Katika ripoti yake, Amnesty ina wasiwasi hasa kwa sababu idara hii limekuwa ikizidisha ukandamizaji wake tangu mwanzo wa mwaka. Shirika hili lisilo la kiserikali linashutumu "kutokujali" kwa ukiukwaji huu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na makundi yenye silaha yanayofanya kazi chini ya uongozi wa jeshi la taifa la Libya linaloongzwa na Marshal Khalifa Haftar.

"Ongezeko la kuzuiliwa kiholela na vifo vizuizini kunaonyesha kwamba utamaduni wa kutoadhibiwa unaruhusu makundi yenye silaha kukiuka haki ya maisha ya wafungwa bila hofu ya adhabu," amesema Bassam Al Kantar, mtaalamu wa Libya katika Amnesty, aliyenukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.