Pata taarifa kuu

Fahamu kwa nini raia wa Libya walifukzwa nchini Afrika Kusini

Nchini Afrika Kusini, maswali yamezuka kuhusu kukamatwa na kufukuzwa nchini humo kwa raia 95 wa Libya. Kwanini walikuja nchini humo na kwa niaba ya nani ?

Jumapili iliyopita, raia hao wa Libya, walirudishwa nyumbani, baada ya kukamatwa Julai tarehe 26, walipobainika kutoa taarifa za uongo kuwa walikuwa wanafunzi waliokuja kutafuta elimu nchini Afrika Kusini.
Jumapili iliyopita, raia hao wa Libya, walirudishwa nyumbani, baada ya kukamatwa Julai tarehe 26, walipobainika kutoa taarifa za uongo kuwa walikuwa wanafunzi waliokuja kutafuta elimu nchini Afrika Kusini. AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumapili iliyopita, raia hao wa Libya, walirudishwa nyumbani, baada ya kukamatwa Julai tarehe 26, walipobainika kutoa taarifa za uongo kuwa walikuwa wanafunzi waliokuja kutafuta elimu nchini Afrika Kusini.

Serikali ya Afrika Kusini inasema, baada ya uchunguzi wao, raia hao wa Libya, walibainika kuwa, walikuwa wanapata mafunzo ya kijeshi kwenye kambi ya siri, katika jimbo la Mpumalanga, linalopakana na nchi ya Msumbiji na Eswatini.

Baada ya kurejea nyumbani, katika mji wa Benghazi, ripoti zinasema, watu hao walitokea Mashariki mwa Libya na ni wafuasi wa kiongozi wa kundi la wapiganaji Khalifa Haftar, anayedhibiti Mashariki mwa nchi hiyo.

Khalifa Haftar, Mbabe wa kivita nchini Libya
Khalifa Haftar, Mbabe wa kivita nchini Libya REUTERS - ESAM OMRAN AL-FETORI

Wakati walipokamatwa, serikali ya Tripoli, inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, inayooongozwa na Abdelhamid Dbeibah ilikanusha kuhusika na mpango wa kuwatuma raia hao nchini Afrika Kusini na kusema, ilikuwa tayari kusaidia kwenye uchunguzi.

Hata hivyo, kiongozi wa waasi Khalifa Haftar amesalia kimya kuhusu sakata hili, lakini serikali anayoongozwa Mashariki mwa Libya, iliteuwa wakili kuwatetea watu hao waliokamatwa nchini Afrika Kusini na kutuma ndege maalum kwenda kuwarudisha nyumbani, baada ya mashtaka dhidi yao kufutwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.