Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Watu wenye silaha waripotiwa kuwashambulia raia na wanajeshi

Kundi la wanajihadi limeripotiwa kuwavamia wanajeshi na raia zaidi ya Elfu Moja nchini Burkina Faso na kuua baadhi yao, kwa mujibu wa taarifa ya gavana Ram Joseph Kafando, wa jimbo la Tawori.

Burkina Faso na mataifa jirani ya Mali na Niger yanaendelea kupambana na wimbi la wanajihadi eneo nzima la sahel.
Burkina Faso na mataifa jirani ya Mali na Niger yanaendelea kupambana na wimbi la wanajihadi eneo nzima la sahel. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Gavana Ram amesema shambulio hilo lilitokea Agosti 9 bila kutoa maelezo zaidi hasa kuhusiana na idadi ya watu waliofaraiki na ikiwa wanajeshi ni baadhi yao.

Burkina Faso na mataifa jirani ya Mali na Niger yanaendelea kupambana na wimbi la wanajihadi eneo nzima la sahel, tangu kuchipuka kwa wanajihadi hao miaka 12 iliopita.

Mataifa ya Ukanda wa Saheli yakiwemo, Mali, Burkina Faso na Niger yametangaza kuundwa kwa muungano wao.
Mataifa ya Ukanda wa Saheli yakiwemo, Mali, Burkina Faso na Niger yametangaza kuundwa kwa muungano wao. © Mahamadou Hamidou / REUTERS

Pametokea mapinduzi mawili ya serikali nchini Mali, mawili nchini Burkina Faso na moja nchini Niger, viongozi walioendesha mapinduzi hayo wakituhumu serikali za awali kwa kukosa  kubaliana na tatizo la usalama kutoka kwa wanajihadi.

Mataifa ya Mali, Niger na Burkina Faso yametangaza kukatisha uhusiano wao na mkoloni wao wa zamani nchi ya Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.