Pata taarifa kuu

DRC: Maafisa kadhaa wa polisi wakimbilia Uganda, M23 yateka kijiji cha Ishasha

Waasi wa M23 wanashikilia tangu Jumapili Agosti 5 udhibiti wa kijiji cha Ishasha, kinachopakana na Uganda, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo usitishaji mapigano ulipaswa kuanza kutekelezwa siku ya Jumapili siku wa manane, kulingana na vyanzo vya ndani.

M23 ni kudi la waasi wengi wao ni Watutsi ambao, wakiungwa mkono na Rwanda, wameteka maeneo makubwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini tangu mwishoni mwa mwaka 2021.
M23 ni kudi la waasi wengi wao ni Watutsi ambao, wakiungwa mkono na Rwanda, wameteka maeneo makubwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini tangu mwishoni mwa mwaka 2021. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ishasha iko bila upinzani chini ya udhibiti wa M23. Waasi ni wengi na wana vifaa vya kutosha", wakati mbapo maafisa wa polisi wa Kongo walikimbilia nchini Uganda, Romy Sawasawa, rais washirika la kiraia huko Ishasha, ameliambia shirika la habari la AFP. Waasi walifanya mkutano na wakaazi ambapo waliwataka "kufanya shughuli zao kwa uhuru", ameongeza.

Pia "waliwaomba Mai-Mai (wanamgambo wanaounga mkono serikali) kuungana nao na FDLR (waasi wa Kihutu wa Rwanda) kurejea nchini mwao Rwanda", kabla ya kuwataka maafisa wa polisi waliokuwa wamekimbia kurejea katika mji huo, Yasini Mambo, mkazi wa Ishasha ameliambia shirika la habari la AFP.

M23 ni kundi la waasi, wengi wao wakiwa ni Watutsi ambao, wanaungwa mkono na Rwanda, na wameteka maeneo makubwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini tangu mwishoni mwa mwaka 2021. Kijiji cha Ishasha kinachopatikana kwenye mpaka na Uganda, kusini mwa Ziwa Edward, iko takriban kilomita 200 kaskazini mashariki mwa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kutekwa kwake kulifanyika siku moja baada ya kuanguka kwa Nyamilima, mji mkubwa jirani, ambao pia uliangukia mikononi mwa waasi bila mapigano, kulingana na wakaazi. Kulingana na mamlaka ya Uganda, makumi ya maafisa wa polisi wa Kongo, waliorudishwa nyuma na M23, walivuka mpaka na kuingia nchini Uganda.

"Tumeoridhesha takriban maafisa 90 wa polisi waliowaliovuka mpaka na silaha zao katika mpaka wa Ishasha, walijitambulisha," naibu mkuu wa idara ya usalama katika wilaya ya Kanungu, nchini Uganda Gad Rugaju aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili. Wilaya ya Kanungu iko kwenye mpaka na DRC na takriban kilomita 10 kutoka Nyamilima.

Polisi hawa “walirudishwa nyuma (Jumamosi) na waasi wa M23 na kwa usalama zaidi, walivuka mpaka wa Ishasha na kupokelewa na kupelekwa kwenye kitengo cha jeshi kwa ajili ya kufanyiwa tathmini na pengine watafukuzwa kwa ufuatiliaji baada ya mashauriano, ” Gad Rugaju aliongeza. Afisa huyu pia alibaini kuwa mamia ya raia waliingia Uganda kupitia Ishasha na kwa sasa wanahudumiwa na mamlaka katika maeneo hayo na shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakiimbizi, UNHCR).

Kama sehemu ya mzozo huu kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23, makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Kinshasa na Kigali, yaliyopaswa kuanza kutumika siku ya Jumapili, yalitangazwa Jumanne na upatanishi wa Angola. Chanzo cha usalama cha Kongo kimethibitisha kutekwa kwa Ishasha na waasi, kulingna na shirika la habari la AFP. 

Eneo lenye utajiri wa madini mashariki mwa DRC limeharibiwa kwa miaka 30 kutokana na mapigano kati ya makundi yenye silaha ya ndani na nje ya nchi, kuanzia vita vya kikanda vya miaka ya 1990.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.