Pata taarifa kuu

Niger: Mkurugenzi wa Gazeti la 'L'Enquêteur' aachiliwa huru kwa muda

Mahakama ya Niger imemuachilia huru kwa muda mkurugenzi wa Gazeti la kila siku la "L'Enquêteur", Idrissa Soumana Maiga, aliyekuwa anazuiliwa tangu mwisho wa mwezi wa Aprili kwa madai ya "kuhatarisha ulinzi wa taifa".

Niger imetawaliwa tangu Julai 26, 2023 na utawala wa kijeshi.
Niger imetawaliwa tangu Julai 26, 2023 na utawala wa kijeshi. © ORTN
Matangazo ya kibiashara

Bw. Maiga "aliachiliwa siku ya Jumanne mchana, yuko nyumbani na amepumzika," amesema Harouna Mamoudou, mhariri wa Gazeti hilo. Amebainisha kuwa Bw. Maiga alinufaika na "kuachiliwa kwa muda", baada ya "miezi miwili na wiki mbili akiwa kizuizini".

Idrissa Soumana Maiga alikamatwa na polisi mnamo Aprili 25 na kuwekwa chini ya ulinzi siku nne baadaye katika gereza la Niamey na jaji anayechunguza faili yake kwa madai ya "kuhatarisha ulinzi wa taifa", ametangaza wakili wake Kafougou Ousmane Ben.

Kulingana na Wakili Ousmane Ben, shtaka la mteja wake lilihusishwa na makala iliyochapishwa Aprili 25 katika Gazeti la L'Enquêteur chini ya kichwa: "Madai ya kuwekwa kwa mitambo ya kunasa maongezi inayodaiwa kuwekwa na maafisa Urusii kwenye majengo ya serikali." "Ni nani hasa wanajaribu kufuatilia na kwa nini?", liliandika Gazeti hili la kila siku.

Mfumo wa Utekelezaji kwa Wataalamu wa Vyombo vya Habari (CAPM), kundi lililoundwa hivi majuzi la wanahabari wa ndani, lilishutumu kukamatwa kwa mkurugezi wa Gazeti hilo na kutaka "kuachiliwa" kwake.

"Data ambayo inaweza kuvuruga utulivu wa umma"

Niger imepoteza nafasi mbili kwa mwaka mmoja katika orodha ya uhuru wa vyombo vya habari duniani iliyotangazwa na shirika la Wanahabari Wasio na Mipaka (RSF), kutoka nafasi ya 59 mwaka 2022 hadi nafasi ya 61 mwaka 2023. Katikati ya mwezi Juni, sheria ya 2019 inayokandamiza usambazaji wa data kidijitali yenye msingi wa kuvuruga utulivu wa umma” imekuwa ngumu na hukumu zinazowezekana kwa wakosaji.

Niger imekuwa ikikabiliwa na ghasia kutoka kwa makundi ya wanajihadi kwa miaka kadhaa, kama vile majirani zake, Burkina Faso na Mali, ambayo pia inatawaliwa na jeshi na ambayo ni sehemu ya shirikisho la AES.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.