Pata taarifa kuu

Wahamiaji 90 wamezama pwani ya Mauritania wakati wakielekea Ulaya

Wahamiaji karibu 90 waliokuwa wanakwenda barani Ulaya, wamepoteza maisha baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kuzama pwani ya nchi ya Mauritania.

Wahamiaji wakiwa ndani ya boti wakiwasili katika bandari ya Arguineguin, katika kisiwa cha Uhispania cha Gran Canaria, Februari 8, 2024. Ofisi ya Kimataifa ya Uhamiaji inasema kivuko cha Mediterania ndicho kilichokuwa njia mbaya zaidi kwa wahamiaji mwaka wa 2023.
Wahamiaji wakiwa ndani ya boti wakiwasili katika bandari ya Arguineguin, katika kisiwa cha Uhispania cha Gran Canaria, Februari 8, 2024. Ofisi ya Kimataifa ya Uhamiaji inasema kivuko cha Mediterania ndicho kilichokuwa njia mbaya zaidi kwa wahamiaji mwaka wa 2023. © Borja Suarez/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa uokoaji nchini Mauritania wanasema, wamefanikiwa kuopoa miili 89 baada ya boti hiyo kuzama kwenye Bahari ya Atlantic Pwani ya mji wa Ndiago.

Watu tisa tu akiwemo mtoto wa miaka mitano ndio waliopatikana wakiwa hai, lakini wengine 72 bado hawajapatikana.

Ripoti zinasema kuwa boti iliyozama, ilikuwa na abiria 170 waliokuwa wametokea nchini Senegal na Gambia.

Raia wengi wa bara Afrika hutumia njia ambazo sio salama kwenda bara Ulaya ambapo maafa huripotiwa.
Raia wengi wa bara Afrika hutumia njia ambazo sio salama kwenda bara Ulaya ambapo maafa huripotiwa. © DESIREE MARTIN / AFP

Hii sio mara ya Kwanza kushuhudiwa kwa ajali kama hizi, ambapo wahamiaji hupitia nchi za Morocco, êneo la Western Sahara, Mauritania, Gambia na Senegal wakilenga kufika Ulaya.

Idadi ya wahamiaji wanaopitia Kaskazini mwa bara la Afrika,  wakilenga kufika katika visiwa vya Canary nchini Hispania ambapo tangu mwaka 2023, idadi hiyo imefikia karibu watu Elfu 40, huku wengine zaidi ya Elfu tano wakipoteza maisha baharini kwa kipindi cha miezi mitano ya mwaka huu wakijaribu kufika nchini Hispania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.