Kilomita kwa saa
Mandhari
(Elekezwa kutoka Km/saa)
Kilomita kwa saa (kifupi: km/h) ni kipimo cha kasi. Km peke yake ni kifupi cha kilomita na h ni kifupi cha saa (kutoka Kilatini hora > Kiingereza hour).
Kitu chenye kasi ya km/h 1 (kilomita moja kwa saa) kinatembea kilomita moja katika muda wa saa moja. Mwanadamu kwa mwendo wa wastani anatembea kwa km/h 5 yaani katika muda wa saa moja anatembea kilomita tano. Kwa kutumia baisikeli kwa kasi ya wastani mtu husafiri kwa km/h 15 hadi km/h 20. Magari yanaruhusiwa kusafiri kwa 50 km/h mijini na 80 hadi km/h 100 nje ya miji.
Kipimo cha SI kwa kasi ni m/s yaani mita kwa sekunde lakini hakitumiki sana kwa sababu katika maisha ya kila siku watu hawataki kujua mwendo wao kwa kila sekunde.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- The converter for speed units: km/h, mph, knots, etc. Archived 9 Mei 2021 at the Wayback Machine.
- A conversion calculator for Units of Speed
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kilomita kwa saa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |