Nenda kwa yaliyomo

Ghuba ya Carpentaria

Majiranukta: 14°00′S 139°00′E / 14.000°S 139.000°E / -14.000; 139.000
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Ghuba ya Carpentaria.
Ghuba ya Carpentaria katika ramani ya Kiholanzi ya mwaka 1859.

Ghuba ya Carpentaria (14°00′S 139°00′E / 14.000°S 139.000°E / -14.000; 139.000) ni sehemu ya bahari kwenye kaskazini ya Australia. Pande za kusini, magharibi na mashariki iko Australia bara, upande wa kaskazini iko Bahari iliyopo baina ya Australia na Guinea Mpya. Kwenye kinywa chake, ghuba ina upana wa km 590, urefu wa kaskazini hadi kusini ni km 700.

Eneo la maji ni takribani km² 300,000. Maji yake huwa na kina kati ya mita 55 hadi 66, ingawa kuna sehemu zenye mita 82. [1]

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Ardhi karibu na ghuba kwa jumla ni tambarare bila miinuko mikubwa. Kisiwa kikubwa ndani yake inaitwa Groote Eylandt.

Tabianchi ni ya joto na unyevunyevu, kuna misimu miwili ya mwaka. Msimu mkavu hudumu kutoka Aprili hadi Novemba na una upepo mkavu sana kutoka mashariki. Msimu wa mvua huanza mwezi wa Disemba ukiendelea hadi Machi. Maeneo mengi kando ya ghuba hujaa mafuriko. Ghuba pia ni eneo la kuzaliana kwa vimbunga vya kitropiki kutoka Novemba na Aprili.

Mito ya Ghuba

[hariri | hariri chanzo]
  1. http://permanent.access.gpo.gov/websites/pollux/pollux.nss.nima.mil/NAV_PUBS/SD/pub175/175sec01.pdf

14°00′S 139°00′E / 14.000°S 139.000°E / -14.000; 139.000