Baktria
Baktria ilikuwa eneo la kihistoria katika Asia ya Kati. Kitovu chake kilikuwa mji wa Balkh katika kaskazini ya Afghanistan ya leo. Inaaminiwa ya kwamba dini ya Uzoroasta ilianzishwa hapa.
Koreshi Mkuu alivamia Baktria manmo 538 KK na kuifanya jimbo la Uajemi. Ilikuwa maarufu kwa farasi zake na rutba ya ardhi. Baada ya mwisho wa milki ya Uajemi ya Kale kutokana na vita za Aleksanda Mkuu Baktria ilikuwa sehemu ya milki ya Waseleuki. Mnamo mwaka 240 KK gavana Mgiriki alitangaza uhuru wa eneo lake na kuanzisha Baktria ya Kigiriki iliyopanukahadi kutwala sehemu zote za Afghanistan ya leo hadi bonde la mto Indus. Lakini Wagiriki wachache walishindwa kuendeleza utawala wao walivamiwa na kushindwa na makabila ya Asia Kati.
Baada ya watawala waliobadilikabadilika hadi uvamizi wa Waarabu tangu mwaka 663. Kuanzia sasa eneo la Baktria ilikuwa sehemu ya milki za Waislamu ikaishia kuwa na historia ya pekee.