Jeri
Mandhari
Jeri | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Jeri koo-michirizi
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 3:
|
Jeri ni ndege wadogo wa jenasi Neomixis katika familia Cisticolidae. Wanafanana na videnenda lakini hawana michirizi mizito. Ndege hawa wana rangi ya kahawa au zaituni mgongoni na nyeupe au kijivu chini na pengine njano pia. Wanatokea misitu ya Madagaska. Hula wadudu. Tago lao ni donge la majani, manyasi na vigoga katikati ya vitawi lenye mwingilio juu kwa upande. Jike huyataga mayai 3-5.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Neomixis striatigula, Jeri Koo-michirizi (Stripe-throated Jery)
- Neomixis tenella, Jeri Koo-njano (Common Jery)
- Neomixis viridis, Jeri Mgongo-kijani (Green Jery)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Jeri koo-njano