Kal Ho Naa Ho
,Kal Ho Naa Ho (matamshi ya Kihindi: [kəl ɦoː naː ɦoː]; tafsiri: Kesho haiwezi kufika; pia ilifupishwa kama KHNH), ni filamu ya Kihindi ya mwaka 2003 iliyoongozwa na Nikkhil Advani. Waigizaji wa filamu hii ni Jaya Bachchan, Shah Rukh Khan, Saif Ali Khan, na Preity Zinta, na Sushma Seth, Reema Lagoo, Lillete Dubey, na Delnaaz Paul katika majukumu ya kusaidia. Filamu hii inasimulia hadithi ya Naina Catherine Kapur, mwanafunzi wa MBA aliyempenda jirani yake Aman Mathur, ambae alikuwa mgonjwa mahututi ambae alijaribu kuweka urafiki baina ya Catherine Kapur na rafiki wake wa karibu sana Rohit Patel, kwani anaogopa atamuumiza Catherine kwa sababu hajui mwisho wake ni lini wa kuishi.
Kutolewa
Kal Ho Naa Ho iliachiliwa mnamo 27 Novemba 2003.
Wahusika
Jaya Bachchan kama Jennifer Kapur, Shah Rukh Khan kama Aman Mathur, Saif Ali Khan kama Rohit Patel, Preity Zinta kama Naina Catherine Kapur (baadaye Patel), Sushma Seth kama Lajjo Kapur, Reema Lagoo kama mama wa Aman, Lillete Dubey kama Jaswinder "Jazz" Kapoor, Delnaaz Paul kama Jaspreet "Sweetu" Kapoor, Shoma Anand kama Kammo, Kamini Khanna kama Vimmo, Ketki Dave kama Sarlaben Patel, Sulbha Arya kama Kantaben, Athit Naik kama Shiv Kapur na Jhanak Shukla kama Gia Kapur
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kal Ho Naa Ho kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |