Emmanuel Myamba
Emmanuel Myamba | |
---|---|
Amezaliwa | Emmanuel Peter Myamba |
Jina lingine | Pastor Myamba |
Kazi yake | Mwigizaji mwongozaji mtayarishaji mchungaji |
Miaka ya kazi | 2005 |
Emmanuel Peter Myamba ni mwigizaji, mwongozaji na mtayarishaji wa filamu kutoka nchini Tanzania. Anafahamika sana kwa kucheza kama mchungaji katika filamu ya Sikitiko Langu ambayo alifanya vizuri na hatimaye kuja kucheza tena uhusika huohuo katika filamu kibao hapo baadaye na Fake Pastors. Myamba ambaye baadaye akaja kuwa mchungaji katika maisha ya kweli. Amefungua kanisa lake huko Kigamboni.[1] Myamba pia amefungua chuo cha mambo ya uigizaji wa filamu kinachoitwa Tanzania Film Training Center na vilevile kampuni ya utengenezaji wa filamu Born Again Film Company inayotengeneza na kusambaza filamu.[2] Baadhi ya filamu alizocheza ni pamoja na Moses, Pastor Myamba Temptation, Saturday Morning, White Maria, Msukule, My Pastor, This Is It, From China With Love, Last Minutes, Penina, Fake Pastors na Dar 2 Lagos.
Baadhi ya filamu alizocheza
- Gods Kingdom
- The Spirit of Miss Marry
- Pasuko la Moyo
- Dangerous Forest
- Pamoja
- My Man
- Cheque in the Bible
- The Promise of Pain
- Queen Spear
- Campus
- Pastor Myamba the Trial
- Ray of Hope
- Bad Saturday
- Shoga Yangu
- Moses
- Pastor Myamba Temptation
- Saturday Morning
- White Maria
- Msukule
- My Pastor
- This Is It
- From China With Love
- Last Minutes
- Penina
- Fake Pastors
- Dar 2 Lagos
Tazama pia
Marejeo
- ↑ Kanisa la Myamba Kigamboni, Dar es Salaam. Mnamo 14 Agosti, 2017.
- ↑ Emmanuel Myamba Archived 29 Mei 2017 at the Wayback Machine. katika Bongo Cinema.com