Namba asilia
Namba asilia (ing. natural numbers) katika hisabati ni namba zinazotumika kwa kuhesabu (kama hivi "kuna sarafu tatu mezani") na kwa kupanga (kama hivi "huu ni mji wa tatu kwa ukubwa hapa nchini"). Katika lugha za Kizungu, maneno yanayotumika kuhesabia huitwa "namba kadinali".
Baadhi ya waandishi huanza kuhesabu namba asilia na 0, wakifuatia na namba kamili zisizo hasi 0, 1, 2, 3...., ambapo wengine huanza na 1, kisha wakifuatia na namba kamili chanya 1, 2, 3..... Maandishi yatokanayo na namba asilia yasiyohusisha sifuri mara nyingine humaanisha namba asilia pamoja na namba nzima, lakini katika maandishi mengine, neno hili linatumika badala ya namba nzima (ikiwa ni pamoja na namba nzima hasi).
Namba asilia ni msingi ambao katika huo makundi mengine ya namba yameundwa kwa kupitia upanuzi: namba nzima, namba kamili, namba wiano, namba halisi na nyingine nyingi. Minyororo hii ya upanuzi hufanya namba asilia (kutambuliwa) katika mifumo mingine ya namba.
Tabia za namba asilia, ni kama kugawanyika na mgawanyiko wa namba tasa, husomwa katika nadharia ya namba.
Katika lugha ya kawaida, kwa mfano kwenye shule ya msingi, namba asilia zinaweza kuitwa namba za kuhesabia, kuelezea utofauti ya namba za kuhesabia na mwendelezo wa vipimo, ulioanzishwa na namba halisi.
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Namba asilia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |