Nenda kwa yaliyomo

Mdororo Mkuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Watu wengi walikosa kazi wakati wa kipindi cha Mdororo Mkuu

Mdororo Mkuu kilikuwa kipindi ambacho uchumi wa Marekani na sehemu zingine za dunia ulikuwa mbaya sana. Ilianza na Kuanguka kwa Soko la Hisa la Marekani 1929. Bei za masoko katika Soko la Hisa la Marekani zilianguka kuanzia tar. 24 Oktoba hadi hapo tar. 29 Oktoba, 1929. Watu wengi sana walipoteza kazi zao. Watu wengi wakawa hawana makazi na maskini. Hii ilimaliza utajiri wa Roaring Twenties. Ile siku ambayo imesemwa kuanzia kwa Mdororo Mkuu inaitwa "Black Tuesday."

Wakati Mdororo Mkuu umeanza, Herbert Hoover ndiye alikuwa rais wa Marekani. Watu walipiga kura kwa ajili ya rais mpya hapo 1932. Jina lake lilikuwa Franklin D. Roosevelt. Roosevelt alivyopata serikali akapata kupitisha sheria mpya na mipangpo ya kusaidia watu ambao walipata kuumizwa na Mdororo Mkuu. Hiyo mipango ilikuwa ikiitwa New Deal. Mdororo Mkuu ulikuwa mbaya sana, lakini kwa msaada wa kila mmoja, imepata kuwa afadhali. Na kila kitu kikaja kuwa sawa. Kati ya 1939 na 1944, watu wengi wakapata kazi tena kwa sababu ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na huo Mdororo Mkuu ukawa unaelekea ukingoni na maisha yakawa kawaida na si kama hapo awali.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdororo Mkuu kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdororo Mkuu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.