Nenda kwa yaliyomo

Utoaji mimba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mimba ya wiki 10 hivi ilitolewa tumboni mwa mama kwa njia ya upasuaji.

Utoaji mimba ni tendo la hiari la kuua mimba iliyokwishatungwa tumboni mwa mwanamke. Unaweza kufanywa naye au na watu wengine kwa kibali chake au bila ya hicho.

Ni tofauti na tukio lisilokusudiwa la mimba kuharibika kwa sababu mbalimbali.

Badala ya kuheshimu kwa shukrani maajabu ya Mungu katika uumbaji, mara nyingi binadamu aliyeshirikishwa naye kazi hiyo, amejifanya muuaji wa watoto wasiozaliwa bado na wa wale waliozaliwa pia.

Sababu zinaweza kuwa mbalimbali: haya, hali ya uchumi, ulemavu, ubaguzi wa jinsia n.k.

Kwa vyovyote Biblia inasema uuaji wa wasio na hatia unamlilia Mungu alipe kisasi, na dini mbalimbali zinapinga vikali tendo hilo.

Kumbe siku hizi katika nchi nyingi utoaji mimba umehalalishwa na mabunge na umekuwa ukichangiwa na serikali.

Kwa njia hiyo kila mwaka watoto milioni mia na zaidi wanaangamizwa kwa ukatili wasizaliwe, bila ya kuhesabu wale wanaouawa na vidonge, sindano, poda, vitanzi na vipandikizi, pengine bila ya wahusika kujua wala kutambua kilichotokea, kwa kuwa hivyo vinatangazwa kama njia za uzazi wa mpango unaopanga upatikanaji wa mimba, kumbe ukweli ni kwamba vinaua mimba zilizokwishaumbwa, mbali ya kwamba vinaharibu afya ya akina mama.

Kuna pia njia nyingine za kuzuia uzazi, kama vile: kumwaga mbegu nje ya tumbo la uzazi, kuvaa mipira ya kiume na ya kike, kufunga kizazi cha mwanamume au cha mwanamke: ingawa njia hizo haziui mimba, zinaleta madhara kwa wanaozifuata, tena zinashindikana kwa kiasi tofauti. Hapo mtu aliyekusudia kukwepa mimba kwa mbinu yoyote anafikia kwa urahisi fulani uamuzi wa kuiua: hivyo hata njia hizo zinaweza zikaandaa njia kwa mauaji ya halaiki.