Nenda kwa yaliyomo

Kipembezo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 12:17, 24 Novemba 2020 na UmojaWetu (majadiliano | michango)
Kipembezo cha kuingia kinaitwa baobonye

Katika utarakilishi, kipembezo (pia: pembezo[1]; kwa kiingereza: peripheral) ni kitumi chote cha tarakilishi ambacho kinatumika ili kuingia na kuondoa taarifa kutoka tarakilishi. Kuna aina kadhaa ya vipembezo.

Kitumi cha kingia ambacho kinaituma data tarakilishi, kama kipanya, baobonye, kamera pembuzi au kitambazo.

Kitumi cha kitolea ambacho kinatoa kitokacho cha tarakilishi, kama kichapishi, kiwambi au kipaza sauti.

Tanbihi

  1. "ENGLISH-SWAHILI DICTIONARY (INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM.)". kamusi.kiswahilipedia.org. Iliwekwa mnamo 2020-11-24.

Marejeo

  • Kiputiputi, O. (2011). Kamusi sanifu ya kompyuta. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, K.602.