Majusi : Tofauti kati ya masahihisho
No edit summary |
d roboti Nyongeza: fa:سه مغ |
||
Mstari 34: | Mstari 34: | ||
[[es:Reyes Magos]] |
[[es:Reyes Magos]] |
||
[[eu:Errege Magoak]] |
[[eu:Errege Magoak]] |
||
[[fa:سه مغ]] |
|||
[[fi:Itämaan tietäjät]] |
[[fi:Itämaan tietäjät]] |
||
[[fr:Rois mages]] |
[[fr:Rois mages]] |
Pitio la 14:55, 22 Agosti 2010
.
Majusi (kutoka Kar. مجوس majus na Kigiriki μάγος (magos), kutoka Kiajemi cha Kale 'magâunô') ni mtaalamu wa nyota katika fani ya unajimu.
Katika matumizi ya kawaida jina hilo linatumika kuwatajia watu wa namna hiyo ambao kadiri ya Injili ya Mathayo (2:1-12) walitokea mashariki kwa Israeli wakifuata nyota ya pekee ili kumfikia Mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa, yaani Yesu.
Walipofika Yerusalemu kwenye ikulu la Herode Mkuu walimfanya afadhaike kwa habari hiyo, lakini walielekezwa Bethlehemu kadiri ya utabiri wa nabii Mika.
Walifika na kumkuta mtoto Yesu akiwa na mama yake, Bikira Maria, wakamtolea dhahabu, ubani na manemane.
Halafu wakaonywa wasimrudie Herode, bali warudi kwao kwa njia nyingine.
Kumbe Herode, alipoona hawarudi, akikusudia kumuua mtoto, aliagiza wauawe watoto wote wa kiume wenye umri chini ya miaka 2 katika eneo la Bethlehemu.
Historia ya neno
Neno la Kiswahili limetokana na Kiarabu مجوس majus lililopokelewa kutoka Kiajemi cha kale kupitia Kigiriki. Kiasili kilimaanisha makuhani wa dini ya Uajemi ya Kale hasa wafuasi wa Zoroaster.
Wagiriki waliamini ya kwamba makuhani hao walikuwa na elimu ya siri hasa kuhusu nyota na utabiri wa nyota. Kwa hiyo katika lugha kadhaa neno limenendelea kumaanisha ama wananajimu au watu waliojua fani za ushirikina.