Nungunungu
Nungu wa Afrika (Hystrix cristata)
Nungu wa Afrika (Hystrix cristata)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia
Nusuoda: Hystricomorpha
Brandt, 1855
Ngazi za chini

Familia 2, jenas 8 (spishi 3 katika Afrika):

Nungunungu au nungu ni wanyama wagugunaji wenye ngozi yenye miiba iliyochongoka wanayotumia kujilinda na maadui. Walienea katika ulimwengu wa sasa na ulimwengu wa zamani. Katika wanyama wagugunaji ni watatu kwa ukubwa, wakitanguliwa na capybara na buku. Nungu wana urefu kati ya sm 20–25. Uzito wao wakaribia kg 5.4–16. Wana umbo la duara, wakubwa na wataratibu kweli. Nungu huwa katika rangi mbalimbali ya kijivu, na mara chache nyeupe. Kujihami kwa miiba kwa nungu hufanana na kule kwa kalunguyeye (Erinaceomorpha) na ekidna (Monotremata).

Spishi

hariri
 
Nungu wa Dunia ya Kale

Nungu ni miongoni mwa spishi 29 za wanyama wagugunaji (rodent) wa familia ya Erethizontidae au Hystricidae. Nungu wanatofautiana kwa ukubwa. Nungu aitwaye Rothschild's Porcupine wa Amerika ya Kusini ana uzito pungufu ya kilo moja; wa Afrika anaweza kukua mpaka kufikia kilo 10. Familia mbili hizi za nungu ni tofauti kabisa na ingawa wote wapo kwenye tawi la Hystricognathi wa oda ya Rodentia, hawahusiani sana. Nungu kumi na moja wa Dunia ya kale, wengi walikuwa ni wa nchi kavu huku wakiwa wakubwa kidogo na wana miiba iliyojikusanya kwa makundi. Inaaminika kuwa wametokana na hystricognaths wengine takribani miaka milioni 30 mapema zaidi kuliko nungu wa dunia ya leo.

Nungu wa dunia ya leo wana umbo ndogo kwa kawaida (japokuwa nungu wa Amerika ya Kaskazini wanafikia kama sm 85 kwa urefu na uzito wa kilogramu 18), huku miiba yao ikiwa imejishikiza mmoja mmoja badala ya kwa makundi na ni wakweaji wazuri, na hutumia muda wao mwingi juu ya miti. Nungu wa dunia ya leo miiba yao ilijitokeza na kukua kwa kujitegemea na wanahusiana zaidi na familia nyingine za wanyama wagugunaji kuliko namna wanavyofahamiana na nungu wa dunia ya kale. Nungu kwa wastani wana uwezo wa kuishi muda mrefu na wanashikilia rekodi miongoni mwa familia yao ya rodent kwa kuishi kwa kiasi cha muda mrefu zaidi,[1] ambayo imevunjwa hivi karibuni na panya aina ya Naked Mole Rat (Heterocephalus glaber).

Miiba ya nungu huchukua sura mbalimbali kulingana na spishi, lakini yote ni nywele zilizoboreshwa na kufunikwa na keratini, na zimejishikiza kwenye misuli ya ngozi. Nungu wa kale (Hystricidae) wana miiba iliyojikusanya kwenye makundi huku kwa nungu wa dunia ya mpya (Erethizontidae), miiba, mmoja mmoja, imechanganyika na ufumwele, manyoya ya chini na nywele.

Miiba huachiwa kwa kuigusa, au hudondoka pale ambapo nungu anajitikisa, lakini hawezi kamwe kurushwa kwa adui, pamoja na imani iliozoeleka. Miiba mipya hukua huchukua nafasi ya ile iliyopotea.

Makazi

hariri

Nungu hupatikana sana katika maeneo ya kawaida na tropiki ya Asia, Italia, Afrika na Amerika ya Kusini na Kaskazini. Nungu huishi kwenye misitu, jangwani sehemu zenye miamba, vilima na nyikani. Baadhi ya nungu wa Dunia Mpya huishi kwenye miti, lakini nungu wa Dunia wa Kale wanakaa ardhini. Nungu huweza kupatikana hata kwenye miamba kwenye ardhi yenye hata urefu wa mita 3700. Nungu ni wanyama wa usiku.

Ulambaji chumvi

hariri

Nungu anapotafuta chumvi wakati mwingine huweza kupata kupitia makazi ya watu na kwa tabaka za mbao zilizopakwa sodium naitreti, rangi za kuta, mishikio ya vifaa, viatu, nguo na vitu vingine vilivyopata jasho. Nungu pia huvutiwa na barabara ambazo chumvi hutumika kuyeyusha barafu, na mara kadhaa huonekana wakilamba magurudumu ya gari zilizopita kwenye barabara hizo. Chumvi maalumu iliyotengwa kama inaweza kuwasaidia wasijiumize.

Vyanzo asili vya chumvi ambavyo nungu hutumia hujumuisha mimea yenye chumvi, mifupa ya wanyama, magamba ya miti, matope kwenye udongo wenye chumvi sana, na vitu vilivyoshikwa na mkojo.

Imani potofu

hariri

Kwa kipindi kirefu nungu huaminika kuwa na uwezo wa kurusha miiba yao kwa adui, hii imekanushwa vikali, baada ya kufahamu kuwa miiba hulegea na kuanguka yenyewe.

Nungu wameanza kufugwa Kenya na wanatumika kama kinweo kwa uzuri kabisa

Uainishaji

hariri
 
Nungu wa Amerika ya Kaskazini akitafuta chakula kwenye nyasi

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri

Marejeo

hariri
  1. Parker, SB (1990) Grzimek's Encyclopedia of Mammals, vol. 4, McGraw-Hill, New York.