Negus
Negus ni cheo cha kifalme katika historia ya Uhabeshi au Ethiopia. Maana ya neno hili ni "mfalme".
Cheo hiki kilitumiwa katika historia ya Ethiopia na watawala mbalimbali wa majimbo kwa mfano wa Shewa, Gonder, Tigray na Gojam. Mtawala mkuu wa Ethiopia alitumia cheo cha "Negus Negesti" (pia: "Negusa Nagast" au mfalme wa wafalme) kinacholingana na "Kaisari".
Negus wa mwisho alikuwa tangu 1928 Ras Tafari Makonnen aliyeendela kuwa Kaisari Haile Selassie I tangu 1930. Alipinduliwa na kuuawa na wanajeshi wa Derg waliomaliza utawala wa kifalme katika Ethiopia.