Muungo kemia
Muungo kemia (kwa Kiingereza: chemical bond) ni kani inayoshikiza atomu, ioni na molekuli na hivyo kuwa msingi wa kutokea kwa kampaundi.
Kani hiyo inaweza kutokana na kani umemetuamo (electrostatic force) katika muungo ionia au na muungo kovalensi ambapo atomu zinashirikiana elektroni.
Muungo wa ioni
haririMuungo ionia unashikiza atomu zake, zinazopatikana kwa umbo la ioni, kutokana na tofauti ya chaji za ioni. Hutokea hasa kwenye chumvi mbalimbali yaani kampaundi za metali na simetali zinazopangwa kwa muundo wa fuwele.
Muungo wa molekuli (kovalensi)
haririElementi simetali zinafanya muungo kwa kushirikiana elektroni kwenye mzingo elektroni wa nje. Atomu zinaelekea kufikia hali ambapo mzingo elektroni wa nje unajaa nafasi zote zinazowezekana. Mfano: atomu sahili ya hidrojeni ina mzingo mmoja wenye elektroni moja tu. Hii ni sababu ya kwamba atomu yake inaungana kirahisi na atomu nyingine ya hidrojeni kuwa molekuli ambapo atomu mbili za hidrojeni zinashirikiana elektroni zake na hivyo kufikia idadi ya juu inayowezekana katika mzingo wa ndani, yaani elektroni mbili. Vivyo hivyo hidrojeni inaungana kirahisi na elementi tofauti ambazo ziko tayari kupokea elektroni yake kwa kukamilisha mzingo wa nje.
Viungo vya nje
hariri- W. Locke (1997). Introduction to Molecular Orbital Theory. Retrieved May 18, 2005.
- Carl R. Nave (2005). HyperPhysics. Retrieved May 18, 2005.
- Linus Pauling and the Nature of the Chemical Bond: A Documentary History Archived 14 Februari 2008 at the Wayback Machine.. Retrieved February 29, 2008.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muungo kemia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |