Mlima Meru
Mlima Meru ni mlima wenye asili ya volkeno na urefu wa mita 4566 (futi 14980) juu ya usawa wa bahari. Mlima huo ni wa tano kwa urefu katika bara la Afrika.
Mlima katika hifadhi ya taifa
haririMlima Meru unapatikana ndani ya Hifadhi ya Arusha ambayo ilianzishwa mwaka 1960 na ambapo wanyamapori kuzunguka Maziwa ya Momella na volkeno ya Ngurudoto (Ngurudoto crater) walihifadhiwa na kulindwa katika eneo hili.
Hifadhi hiyo ina ukubwa wa kilometa za mraba 137 na ipo umbali wa kilometa 35 kutoka mji wa kitalii wa Arusha na Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro.
Jina la mlima huu limetokana na kabila maarufu nchini Tanzania la Wameru ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi na kuuzunguka mlima huu.
Vivutio katika hifadhi hiyo vinajumuisha volkeno, maziwa, misitu na wanyamapori kama twiga, tembo, pundamilia, nyati na wengine wengi. Pia kuna ndege wa aina nyingi wakiwemo flamingo, na misitu katika mlima Meru ni makazi ya nyani.
Kupanda Mlima Meru kunachukua siku tatu hadi nne na wakati mzuri kwa kupanda mlima ni kuanzia mwezi Juni hadi Februari ambapo mvua zinaweza kunyesha katika mwezi Novemba. Na wakati mzuri wa kuona mlima Kilimanjaro kutokea Meru ni kati ya Desemba na Februari.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
haririMajarida ya Utalii na maliasili za Tanzania
Picha
hariri-
Mlima Meru kutoka juu
-
Mlima Meru
-
Kilele cha Mlima Meru (m 3,820)
-
Kilele kingine (m 4,562)
-
Mto kutoka Mlima Meru
-
Ramani ya Mlima Meru
-
Pambazuko kutoka Mlima Mrefu kuelekea Mlima Kilimanjaro
Viungo vya nje
hariri- Mlima Meru katika tovuti ya Geonames
- Utalii wa Tanzania Archived 13 Januari 2010 at the Wayback Machine.
- maliasili za Tanzania
- Mlima meru Archived 15 Juni 2012 at the Wayback Machine.
- Meru
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mlima Meru kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |