Mkoa wa Katavi
Mkoa wa Katavi ni mmojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 50000. Ulianzishwa rasmi mnamo Machi 2012 kwa kumega mkoa wa Rukwa.
Mkoa wa Katavi | |
Location in Tanzania | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Kanda | Nyanda za Juu ua Kusini |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | Rajab Mtumwa |
Eneo | |
- Jumla | 45,843 km² |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 1,152,958 |
EAT | (UTC+3) |
Msimbo wa posta | 50xxx |
Kodi ya simu | 025 |
Tovuti: katavi.go.tz |
Makao makuu yako Mpanda.
Wilaya
Wilaya za mkoa huo ni tano tu: Mlele, Nsimbo, Mpanda mjini, Tanganyika (awali Mpanda vijijini) na Mpimbwe.
Wakazi
Katika sensa ya mwaka 2022 idadi ya wakazi ilihesabiwa kuwa 1,152,958 [1].
Utamaduni
Kabila kubwa ni lile la Wafipa; pia kuna Wabende, Wapimbwe na Wakonongo na dini yao kwa kiasi kikubwa sana ni Ukristo wa madhehebu ya Kanisa Katoliki.
Wapimbwe wanapatikana katika maeneo ya wilaya ya Mpimbwe katika vijiji vya Mamba, Mpimbwe na Majimoto. Katika kijiji cha Mamba kuna kivutio kizuri: bwawa kubwa la asili la maji ya moto ambayo hayapoi muda wote, ni ya moto iwe mchana au usiku.
Pia kuna sehemu za mkoa huu ni wa kihistoria katika baadhi ya maeneo. Mfano mtaa wa Madukani ambao walikua wakiishi Wahindi na Waarabu wa Oman kama Mzee Yusuf Al Salmi.
Majimbo ya bunge
Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Katavi : mbunge ni Issack Kamwele (CCM)
- Kavuu : mbunge ni Dk. Pudenciana Kikwembe (CCM)
- Mpanda Mjini : mbunge ni Sebastian Kapufi (CCM)
- Mpanda Vijijini : mbunge ni Moshi Selemani Kakoso (CCM)
- Nsimbo : mbunge ni Richard Mbogo (CCM)
Tazama pia
Marejeo
Viungo vya nje
- Taarifa juu ya majimbo ya Katavi kabla ya uchaguzi mkuu 2015 (tovuti ya facebook)
- Katavi Postcodes Ilihifadhiwa 28 Agosti 2012 kwenye Wayback Machine.
Viungo vya nje
- Serikali ya Tanzania
- Historia ya Mkoa wa Katavi (machache tu kwenye tovuti ya mkoa wenyewe)
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Katavi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |