Mashapo
Mashapo (kwa Kiingereza: sediment) ni vipande vidogo vya mata thabiti vilivyovunjika na nguvu za maji, barafu, upepo, kwa njia ya mmomonyoko na mabadiliko ya halijoto, halafu kusafirishwa na maji, barafu, upepo au mvuto wa graviti.
Vipande hivyo vilivyovunjika hutokea kama matope, mchanga na mawe. Vikisafirishwa na maji ya mto vinabaki chini baadaye, wakati nguvu ya maji inapungua. Sehemu kubwa inafika baharini; kiasi cha mashapo yote kutoka mito yanayoishia baharini ni vigumu kukitaja kwa uhakika, kiliwahi kukadiriwa kuwa tani 13.5-15 x 10 (tani bilioni 15)9[1] hadi tani bilioni 20[2] kwa mwaka.
Hasa katika maeneo ya mafuriko ya kujirudia mashapo yaliyobaki hufunikwa tena na mashapo mapya ambayo kwa njia hiyo yanaweza kujenga matabaka manene ya ardhi au ya mawe. Katika muda wa milioni za miaka matabaka hayo ya mashapo yanaweza kubadilishwa kuwa mwamba mashapo.
Mashapo ya matope matupu yanaweza kuunda ardhi nzuri ya mashamba, au udongo wa mfinyanzi unaoweza kuendelea kubadilika kuwa mwambatope kama grife. Mashapo ya mchanga husababisha kutokea kwa ufuko wa mchanga baharini, au matabaka ya mchanga yanayochimbwa kwa mahitaji ya ujenzi. Vivyo hivyo kokoto na mawe madogo ambayo mara kwa mara yanapatikana kwa wingi katika sehemu zilizokuwa zamani njia za mito.
Tanbihi
hariri- ↑ John D. Milliman & Robert H. Meade: World-Wide Delivery of River Sediment to the Oceans, The Journal of Geology Vol. 91, No. 1 (Jan., 1983), pp. 1-21
- ↑ John N. Holeman: The Sediment Yield of Major Rivers of the World Archived 3 Desemba 2019 at the Wayback Machine., Water Resources Research, First published: August 1968 https://doi.org/10.1029/WR004i004p00737
Marejeo
hariri- Prothero, Donald R.; Schwab, Fred (1996), Sedimentary Geology: An Introduction to Sedimentary Rocks and Stratigraphy, W. H. Freeman, ISBN 978-0-7167-2726-2
- Siever, Raymond (1988), Sand, New York: Scientific American Library, ISBN 978-0-7167-5021-5
- Nichols, Gary (1999), Sedimentology & Stratigraphy, Malden, MA: Wiley-Blackwell, ISBN 978-0-632-03578-6
- Reading, H. G. (1978), Sedimentary Environments: Processes, Facies and Stratigraphy, Cambridge, Massachusetts: Blackwell Science, ISBN 978-0-632-03627-1
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mashapo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |