Kipanya
Kipanya-nyumbani
Kipanya-nyumbani
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Familia ya juu: Muroidea (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Murinae
Jenasi: Mus
Linnaeus, 1758
Spishi: Angalia katiba

Kutoka Wikipedia, ensaiklopidia huru

Vipanya wa mwituni (field mouse)

Kipanya hupatikana katika oda ya wagugunaji (Rodentia). Spishi inayofahamika sana ni kipanya-nyumbani (Mus musculus). Pia ni mfugo maalum. Kwenye maeneo mengine, vipanya huwa maarufu. Wagugunaji hawa huliwa na ndege wakubwa kama vile vipanga na kozi. Wanafahamika kwa kuhamia makazi ya watu kutafuta chakula na makazi yao. Japo wakifugwa vipanya hawa huweza kuishi kwa miaka miwili na nusu, kwa kawaida vipanya huishi kwa wastani wa miezi minne huko porini, kumpakakana na kuwinda mara kwa mara. Jamii za paka, mbwa-mwitu, bweha, ndege mbua, nyoka na hata jamii fulani za artropoda huwawinda sana vipanya. Hata hivyo humpakakana uwezo wao mkubwa wa kuishi mazingira mbalimbali, vipanya huonwa kuwa ndio jamii ya pili kuishi duniani yenye uwezo mkubwa wa kudumu mazingira baada ya binadamu.

Vipanya huweza kuwa waharibifu, kwa kula na kuharibu mazao[1], kusababisha uharifu wa vifaa na kusambaza magonjwa kupitia vijidudu vyao na kinyesi chao[2]. Kimsingi vipanya ni wanyama wa usiku na hufidia uwezo wao wa kuona kidogo kwa uwezo wao maridadi wa kunusa na kusikia vizuri katika kupata chakula na kuwatambua maadui zao. [3] Vipanya na wenzao panya ndio hasa chachu ya kuanza kufugwa kwa paka ambao kusudi lao ni kuwinda panya hao.


 
Watoto wa kipanya wakiwa na umri wa siku moja.

Kuzaliana

hariri

Uwezo wao wa kuzaaa huwaza pale wanapokuwa na siku 50, japo kipanya jike huweza kuanza kupata hedhi yao ya kwanza wakiwa na siku 25 hadi 40. Vipanya huzaliana mwaka mzima huku mayai yao yakiwepo muda wote. Siku za mzunguko wa mayai huwa ni 4 mpaka 5 na hedhi hudumu kwa masaaa 12 kuanzia jioni. Harufu za uke wao hutambua kusaidia hatua ya mzungoko wa uzazi alionao jike hivyo kujua muda sahihi wa kujamiiana. Vipanya hupandana usiku na hudhibitishwa/ huwezekana kwa kushikwa shahawa kwenye uke kwa saa 24 kwa ujumla. Uwepo kwa manii kwenye uke pia ni alama mojawapo ya kujamiiana. Vipanya hubeba mimba kwa muda wa siku 20. Huzaa wampakampaka takribani 10 - 12 kwa uwezo wa kawaida wenye uzimpaka wa kilogramu 0.5- 1.5, walio na nywele huku masiiona. Macho yao yakiwa yamefunga wampakampaka huachishwa kunyonya baada ya majuma 3, na baada ya siku 2-5, jike hurudia mzunguko wake wa uzazi.

Vipanya wa maabara

hariri
 
Vipanya “Knockout mice”

Vipanya hutumika sana kwenye tafiti za maabara sababu zao ni mamalia na wanamahusiano makubwa sana na binadamu kuliko hata panya wakawaida. Vipanya hutumika sana kama kifani cha binadamu. Sababu nyingine inayowafanya panya hawa watumike maabara ni udogo wao, hawana gharama na ni rahisi kuwatunza huku pia wakizaliana kwa kasi. Vipanya huwa wasikivu sana hasa pale wanapokuzwa na kufuzwa tangu wakiwa wadogo na kama wanapewa sana uangalizi mkubwa wa binadamu, japo baadhi yao wanaonekana kuwa ni wakorofi sana. Panya wa kawaida na vipanya wana kila ogani sawa isipokuwa tu zinampakafautiana kwa ukubwa.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri
  • Mus (Coelomys) crociduroides (Western Sumatra)
  • Mus (Coelomys) mayori (Sri Lanka)
  • Mus (Coelomys) pahari (Northeastern India mpaka southwestern Cambodia na northern Vietnam)
  • Mus (Coelomys) vulcani (Western Java)
  • Mus (Mus) booduga (Pakistan, India, Sri Lanka, Bangladesh, southern Nepal, central Myanmar)
  • Mus (Mus) caroli (Ryukyu islnas, Taiwan na southern China mpaka Thailna; Malaysia na western Indonesia)
  • Mus (Mus) cervicolor (Northern India mpaka Vietnam; mpaka Sumatra na Java)
  • Mus (Mus) cookii (Southern na northeastern India na Nepal mpaka Vietnam)
  • Mus (Mus) cypriacus (Cyprus)
  • Mus (Mus) majorius (Athens, Greece)
  • Mus (Mus) famulus (Southwestern India)
  • Mus (Mus) fragilicauda (Thailand na Laos)
  • Mus (Mus) macedonicus (Balkans mpaka Israel na Iran)
  • Mus (Mus) musculus (introduced worldwide)
  • Mus (Mus) nitidulus (Central Myanmar)
  • Mus (Mus) spicilegus (Austria mpaka southern Ukraine na Greece)
  • Mus (Mus) terricolor (India, Nepal, Bangladesh, Pakistan; introduced mpaka Sumatra)
  • Mus (Pyromys) fernnaoni (Sri Lanka)
  • Mus (Pyromys) phillipsi (Southwestern India)
  • Mus (Pyromys) platythrix (India)
  • Mus (Pyromys) saxicola (Southern Pakistan, southern Nepal, na India)
  • Mus (Pyromys) shortridgei (Myanmar mpaka southwestern Cambodia na northwestern Vietnam)

Kama mfugo wa nyumbani

hariri
 
Vipanya wakifugwa

Watu wengi hununua vipanya kama mfugo wa nyumbani. Wanaweza kucheza, kupendwa na kukua huku ukiwamudu. Hatahivyo hawapaswi kuachwa bila maangalizi sababu wana maadui wengi wa asili, tukijumuisha paka, ndege na mbwa n.k. Kipanya dume huwa na harufu kali kuliko jike. Wakiangaliwa vizuri, huweza kuwa mifugo ya ndani ya nyumba nzuri kwelikweli.

Chakula

hariri

Kwa kawaida vipanya ni wala majani (hebivora), wakila aina yeyote ya matunda au nafaka.[4]. Kutokana na hii vipanya wanafahamika sana kwa kufanikiwa kuishi kwenye mazingira ya watu kwa kula kwa wastani mabaki yeyote ya chakula. Wakifunzwa, hulishwa kwa chakula chao maalum. Vipanya hula chakula chenye uzito mpaka wa gramu 15 kwa gramu 100 za uzito wao kwa siku.

kama chakula

hariri

[5] Vipanya aina ya "Pinkie" wakiuzwa kama chakula cha reptilian

Vipanya huliwa sana na wanyama wengi wala nyama,tangu hapo zamani na mpaka sasa panyapori wamekuwa wakitumiwa kama kimpakaweo.mashariki mwa Zambia na kaskazini mwa Malawi, kama vile huko asia ingawa kwa sasa hawatumiwi sana na binadamu.walikuwa ni chanzo kizuri sana cha protini. Katika nchi kadhaa vipanya wanatumika kama chakula cha mifugo mingine kama vile nyoka, mijusi, chura, na ndege kadhaa. Baadhi ya nchi kama vile Ujerumani, Uingereza n.k. wamepiga marufuku kitendo hiki kwa kuona kimaadili hakifai kwani hujumuisha ukatili.