Injini (kutoka Kilatini ingenium kupitia Kiing. engine) ni mashine inayobadilisha nishati kuwa mwendo unaotumiwa kwa kazi mbalimbali.

Injini ya mvuke ya kuchezea kwa watoto. Fueli inachomwa chini yake, maji kwenye tangi inaanza kuchemka na kuwa mvuke. Shindikizo la mvuke linasukuma pistoni buluu inayozungusha gurudumo tegemeo

Mifano ni

na zote zinabadilisha nishati husika kuwa mwendo wa kuendesha mashine, magari na vifaa mbalimbali.

Vitangulizi vya injini

hariri

Tangu kale watu waliwahi kubuni machine mbalimbali zilizobadilisha nishati kuwa mwendo unaohitajika.

Vitangulizi hivi vya injini vilitumia nguvu ya watu, ya wanayama, maji ya mtoni au upepo.

Hasa mashine za kusaga kama kinuupepo au kinumaji zilitumiwa kwa karne nyingi.

Injini za pistoni

hariri

Chanzo cha injini za kisasa kilikuwa injini ya mvuke tangu karne ya 18. Injini hizi za kwanza zilitumia joto la moto uliowaka nje ya injini yenyewe kwa kusudi la kupata mvuke yenye shindikizo kubwa. Mvuke ulipelekwa ndani ya mabomba hadi silinda iliposukuma pistoni na kusababisha mwendo wa injini. Injini ya mvuke jinsi ilivyobuniwa na James Watt ilitumiwa mwanzoni kabisa kuendesha pampu ya maji katika migodi ya makaa, baadaye pia kwa ajili ya mashine za viwandani na usafiri kama vile meli na gari la moshi.

Nafasi ya injini ya mvuke ilichukuliwa baadaye na injini za mwako ndani zinazochoma fueli ndani yao hasa petroli, diseli, gesi au alikoholi.

Injini hizi huwa na munndo mbalimbali kama vile injini ya mapigo mawili, manne au sita. Vilevile kuna idadi tofauti ya silinda kati ya 1 na 12.

Injini za rafadha

hariri
 
Rafadha ya meli

Mwendo wa gesi ya joto inatumiwa kuzungusha rafadha sawa na upepo unaozungusha mikono ya kinuupepo.

Rafadha za kwanza zilisukumwa na mvuke lakini baadaye gesi za kuchoma fueli mbalimbali zilichukua nafasi ya mvuke.

Injini za jeti kwenye eropleni hutumia aina ya rafadha.

Injini za roketi

hariri
 
Jeti za gesi joto zasukuma roketi

Roketi inatembea kwa sababu gesi yenye shindikizo kubwa inatoka kwenye nyuma yake kwa nguvu.

Gesi inaweza kubanwa ndani ya roketi kwa shindikizo kubwa ikitoka kwenye nozeli inayofunguliwa. Kimsingi kuruka kwa puto ya mpira iliyopulizwa hewa ndani yake lakini haikufungwa ni saswa na mfumo wa roketi.

Kwa kawaida roketi hujaa fueli fulani inayoshomwa kwenye sehemu maalumu kwenye mwisho wake na gesi joto zatoka kwenye nozeli ya nyuma.

Kimitambo roketi ni mashine ya kimsingi sana lakini huwa kati ya injini zenye nguvu kubwa kabisa. Roketi huwa na uwezo kufaya kazi hata kwenye anga-nje.

Injini za umeme

hariri
 
Injini ya umeme

Injini ya umeme haihitaji fueli bali inatumia umeme unaofika kwa njia ya nyaya. Mara nyingi nguvu ya umeme inatokana na fueli iliyochomwa kwenye kituo cha umeme mbali na injini yenyewe.

Ndani ya injini umeme huwasha sumaku kwa namna ya kugeuza pini ya injini.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.