Horst Störmer
Horst Ludwig Störmer (amezaliwa 6 Aprili 1949) ni mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani akiwa ni profesa nchini Marekani. Hasa anajulikana kwa kugundua kanuni fulani ya kifizikia (kwa Kiingereza: quantum Hall effect). Mwaka wa 1998, pamoja na Robert Laughlin na Daniel Tsui alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
Makala hii kuhusu mshindi wa Tuzo ya Nobel bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Horst Störmer kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |