Freeman Mbowe
Freeman Aikaeli Mbowe (amezaliwa 14 Septemba 1961) ni mwanasiasa Mtanzania, mwanachama na mwenyekiti wa Chama cha kisiasa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Alichaguliwa tangu mwaka 2000 hadi 2020kuwa mbunge wa Jimbo la Hai lililopo mkoa wa Kilimanjaro. [1] [2]
Alikuwa mmoja wa waasisi wa CHADEMA mwaka 1992. Mbowe anafahamika kuwa mpangaji mahiri wa mikakati, na hivyo kumfanya kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa siasa nchini.[3]
Mnamo mwaka 2005 Mbowe aliwania urais wa Tanzania kupitia chama chake cha CHADEMA na kuambulia asilimia 5.88 ya kura zote. [4]
Mnamo Julai 2021, alikamatwa pamoja na wanachama wengine kumi waliondoka kwenda Mwanza ambapo walikuwa wakipanga mkutano wa kudai katiba mpya. Hapo alikamatwa na kushtakiwa kuandaa ugaidi kwa lengo la kutumulia serikali.
Tarehe 4 Machi 2022, mashtaka yote dhidi yake yalifutwa akaachwa huru.[5]
Marejeo
hariri- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
- ↑ "Masauni saga exposes CCM's vetting failure", The Citizen, Mwananchi Communications, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-24, iliwekwa mnamo 21 Mei 2010
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://www.dw.com/sw/freeman-mbowe/t-43237526
- ↑ https://peoplepill.com/people/freeman-mbowe/
- ↑ https://twitter.com/AFP/status/1499666122299559937?t=t3lOF96bh7qR9RsheWIodQ&s=19
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |