Eswatini (jina rasmi tangu mwaka 2018 ni Umbuso weSwatini; kifupi cha Kiswati: eSwatini[1]; kwa Kiswahili pia: Uswazi) ni nchi ndogo ya Kusini mwa Afrika isiyo na pwani katika bahari yoyote.

Ufalme wa Eswatini
Umbuso weSwatini (Kiswazi)
Kingdom of Swaziland (Kiingereza)
Kaulimbiu ya taifa: Siyinqaba (Kiswazi)
"Sisi ni ngome"
Wimbo wa taifa:
Nkulunkulu Mnikati wetibusiso temaSwati
"Mungu, Mpaji wa Baraka kwa Waswati"
Mahali pa Eswatini
Mahali pa Eswatini

Mahali pa Eswatini
Ramani ya Eswatini
Ramani ya Eswatini

Ramani ya Eswatini
Miji mikuuMbabane (serikali)
Lobamba (bunge)
Mji mkubwa nchiniMbabane
26°19′ S 31°08′ E
Lugha rasmiKiswati
Kiingereza
Makabila (asilimia)84 Waswati
10 Wazulu
6 wengine

Imepakana na Afrika Kusini na Msumbiji.

Miji mikuu ni Mbabane na Lobamba.

Historia

hariri

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani.

Katika karne za kwanza BK walifika wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi.

Waswati walianzisha ufalme wao katikati ya karne ya 18 chini ya Ngwane III; mipaka ya sasa ilikubalika mwaka 1881.

Baada ya vita kati ya Waingereza na Makaburu, Swaziland ilukuwa nchi lindwa ya Uingereza tangu mwaka 1903 hadi 1967.

Chini ya mfalme Sobhuza II aliyetawala kwa muda mrefu sana (1921-1982), Swaziland ilipata uhuru tarehe 6 Septemba 1968.

Eswatini inatawaliwa tangu mwaka 1986 na mfalme Mswati III. Mfalme anapingwa mara nyingi kwa sababu anatumia pesa nyingi kwa ajili yake binafsi ilhali wananchi ni maskini sana. Kwa muda mwingi wa uhuru wa nchi katiba imesimamishwa, na mfalme ametawala peke yake.

 
Mwanamke kutoka Eswatini akicheza.

Wakazi wengi ni wa kabila la Waswati na kuongea lugha ya Kiswati ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kiingereza. Shuleni kinafundishwa pia Kireno.

Upande wa dini, 89.3% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, hasa Waprotestanti, lakini pia Wakatoliki (5%). Wanaoendelea kufuata dini asilia za Kiafrika ni 0.5% na Waislamu ni 1%.

Eswatini ni kati ya nchi duniani zilizoathiriwa zaidi na Ukimwi; umri wa wastani unafikia miaka 22 pekee kwa sababu ya vifo vingi (64%) vinavyotokana na ugonjwa huo uliopata 26% ya watu wazima wote.

Tanbihi

hariri
  1. Swaziland king renames country 'the Kingdom of eSwatini', tovuti ya BBC, iliangaliwa Aprili 2018

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Eswatini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.