Abdallah Possi

Balozi
(Elekezwa kutoka Abdallah Saleh Possi)

Dk. Abdallah Saleh Possi (amezaliwa 25 Agosti 1979) ni balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani. Amekubaliwa pia kama balozi huko Austria, Bulgaria, Ucheki, Ukulu mtakatifu, Hungaria, Poland, Romania na Uswisi. [1]

Dr Abdallah Saleh Possi


Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani
mtangulizi Philip Sang'ka Marmo

tarehe ya kuzaliwa 25 Agosti 1979 (1979-08-25) (umri 45)
Dar es Salaam, Tanzania
utaifa Mtanzania
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (LL.B., LL.M.)
Chuo Kikuu cha Erlangen–Nuremberg (Uzamivu)

Kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi, Dk Possi aliwahi kuwa mbunge wa chama cha kisiasa cha CCM kwa uteuzi wa rais kwa miaka 20152020, tena naibu waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu. [2]

Hapo awali, alifanya kazi kama mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dodoma nchini Tanzania. Alikuwa pia wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na mkufunzi katika Taasisi ya Tawala za Mahakama huko Lushoto, Tanga, Tanzania.

Ana LL. B. na LL. M. kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na shahada ya uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Erlangen-Nuremberg huko Ujerumani.

Vitabu vyake

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri

Mabalozi wa Tanzania