Zanzibar (Jiji)

Pitio kulingana na tarehe 12:13, 28 Oktoba 2011 na Vagobot (majadiliano | michango) (r2.7.2) (roboti Nyongeza: sk:Zanzibar (mesto))


Jiji la Zanzibar ni mji mkubwa wa kisiwa cha Unguja na mji mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, pia ni wilaya katika Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi wa Tanzania.

Jiji la Zanzibar
Jiji la Zanzibar is located in Tanzania
Jiji la Zanzibar
Jiji la Zanzibar

Mahali pa mji wa Zanzibar katika Tanzania

Majiranukta: 6°9′36″S 39°12′0″E / 6.16000°S 39.20000°E / -6.16000; 39.20000
Nchi Tanzania
Mkoa Unguja Mjini Magharibi
Wilaya Unguja Mjini
Beit-al-Ajaib (1907)

Jiji lina wakazi 206,292 (sensa ya 2002)[1].

Kitovu cha kihistoria ni Mji Mkongwe (Stone Town) ulioandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage). Nyumba za Mji Mkongwe zilijengwa tangu 1830 wakati Sultani Sayyid Said alipohamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja Unguja. Kati ya majengo maarufu ni Beit al Ajaib (nyumba ya maajabu), boma la kale, Kanisa Kuu la Kianglikana kwenye mahali pa soko la watumwa na hasa nyumba nyingi za kihistoria za ghorofa zilizojengwa na famila za tabaka ya matajiri Waarabu zenye milango yenye mapambo mazuri.

Mji Mkongwe unapokea watalii wengi kila mwaka.

Mji wa kisasa umekua sana ngambo ya Mji Mkongwe.


Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu maeneo ya Unguja bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Zanzibar (Jiji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
  Kata za Wilaya ya Mjini Unguja - Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja - Tanzania  

Amani | Banko | Chumbuni | Gulioni | Jang'ombe | Karakana | Kidongo Chekundu | Kikwajuni Bondeni | Kikwajuni Juu | Kilimahewa Bondeni | Kilimahewa Juu | Kilimani | Kiponda | Kisimamajongoo | Kisiwandui | Kwaalimsha | Kwaalinatu | Kwabintiamrani | Kwahani | Kwamtipura | Kwamtumwajeni | Kwa Wazee | Magomeni | Makadara | Malindi | Mapinduzi | Maruhubi | Masumbani | Matarumbeta | Mboriborini | Mchangani | Meya | Miembeni | Migombani | Mikunguni | Mitiulaya | Mkele | Mkunazini | Mlandege | Mnazimmoja | Mpendae | Muembeshauri | Muembetanga | Muungano | Mwembeladu | MwembeMadema | Mwembemakumbi | Nyerere | Rahaleo | Saateni | Sebleni | Shangani | Shaurimoyo | Sogea | Urusi | Vikokotoni


 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: